Uchaguzi 2020 Bango la Magufuli limenishangaza sana

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
Kuna bango moja la Mgombea wa kiti cha Urais, Mh. Magufuli linasema eti Magufuli ni mnyenyekevu!

Nilipoliona bango hili, nikashtuka sana. Nikajiuliza maswali mengi:

1) Ni Magufuli mwenyewe amehiari kuwepo kwa bango la namna hiyo?

2) Kuna watu fulani wameamua kutengeneza bango hilo, labda kwa kumdhihaki Magufuli?

3) Au Magufuli amewaeleza kuwa endapo akichaguliwa safari hii anataka awe mnyenyekevu?

Kuwa 'mnyenyekevu' au kwa kiingereza kuwa 'humble', tafsi yake:

Unyekenyekevu hutokana na neno kunyenyekea. Anayenyenyekea huitwa mnyenyekevu. Kama Magufuli ni mnyenyekevu, ni lazima tujiulize, huwa anamnyenyekea nani?

Kunyenyekea ni kujishusha. Kunyenyekea ni kuamini wewe si kitu mbele ya yule unayemnyenyekea. Kunyenyekea ni kuonesha kuwa ama wewe ni duni mbele ya yule unayemnyenyekea au zaidi ni kuwa upo sawa na yule unayemnyenyekea.

Kunyenyekea maana yake ni kuwa msikivu. Kunyenyekea ni kuwa tayari kupokea ushauri, maelekezo na matakwa ya unaowanyenyekea.

Sasa tujiulize, hivi kweli Rais Magufuli anazo hizi sifa? Bila ya kutafuta majibu toka kwa watu wengine, nina hakika Magufuli hatakuwa amependezwa na bango linalosema yeye ni mnyenyekevu maana mara kadhaa kwa kauli yake na kwa matendo yake amekataa kabisa kuitwa "mnyenyekevu".

Rais Magufuli amewahi kutamka yafuatayo:

1) Mimi sibadilishwi na yeyote, mimi jiwe. Maana yake yeye hapokei ushauri wala maelekezo kutoka kwa yeyote

2) Mimi ukinishauri, ndiyo umeharibu kabisa, maana sitafanya unachonishauri

3) Wewe Mpina ni kichaa mwenzangu, endelea hivyo hivyo

Mtu mnyenyekevu, ni mtu mwenye huruma, kwa sababu anaamini kuwa wale anaowanyenyekea wanastahili kuthaminiwa na kuheshimiwa utu wao.

Mara kadhaa Rais Magufuli amefisha utu wa watu wengine na kuwaonesha kuwa ni takataka mbele yake. Baadhi ya kauli na matendo yake:

1) Huyu Kabudi na Mpango, hawawaambii tu, nilikwishawaambia ni mapumbavu mara nyingi tu

2) Huko Marekani ulikokuwa ulikiwa unafanya upumbavu huu (aliambiwa mkurugenzi wa halmashauri ya Tunduru)

3) Kuna watu walikuwa wanaishi kama malaika, nitahakikisha wataishi kama mashetani (anapenda watu wateseke. Wala hakusema kuwa kuna watu wanaishi kama mashetani, nataka nao waishi kama malaika. Yeye anapenda watu wapate taabu)

4) Kwenye utawala wangu, tajiri anaweza kufanywa chochote wakati wowote (maana yake anaweza kumwonea mtu kwa sababu tu ni tajiri. Yaani kuonesha kuwa yeye ni bora kuliko watu wote kiasi cha kuweza kumfanya mtu chochote bila ya kujali mtu huyo ana kosa au hana kosa)

5) Wa Mwanza msiwabomolee nyumba zao kwa sababu walinipa kura nyingi (kama hukumpa kura, ina maana ni halali kubomolewa nyumba yako. Haamini kuwa kuna mtu mwingine yeyote mwenye haki sawa na ya kwake ya kuweza kupigiwa kura)

6) Kamdai maji mbunge wako uliyemchagua au mume wako (alitamka Tunduma dhidi ya mama aliyemwambia wana tatizo la maji)

7) Ninyi mlichagua mbunge mpinzani ndiyo maana siwezi kuleta maendeleo (aliwaambia wananchi wa kule Lindi)

8) Tetemeko halikuletwa na Serikali wala CCM. Hakuna serikali inayowajengea nyumba wahanga wa matetemeko (aliwaambia wahanga wa tetemeko la ardhi)

9) Serikali haina shamba (aliwaambia wananchi waliomba chakula baada ya mazao yao kufa kwa ukame)

Magufuli anaamini kuwa wananchi wengine ni duni kuliko yeye, hawastahili kuwa viongozi, bali yeye na wale tu ambao yeye anawataka.

Ukimtazama Magufuli, matendo yake na kauli zake, bila ya ushabiki, ungeweza kumtafsiri kwa majumuisho yafuatayo:

1) Ni kiongozi mbabe
2) Ni kiongozi mwenye majivuno
3) Ni kiongozi anayejiamini kupita kiasi
4) Ni kiongozi mwenye dharau
5) Ni kiongozi asiyependa kusikiliza, kuelekezwa wala kushauriwa
6) Ni kiongozi asiye na huruma
7) Ni kiongozi asiyejali

Na kila moja katika hizi sifa 7, kuna au kauli au matendo yanayotoa uthibitisho. Anaweza kuwa na tabia nyingine pia lakini kunaweza kusiwepo na uthibitisho wa moja kwa moja.

Swali langu, hivi kusema Rais Magufuli ni "mnyenyekevu", walioandaa bango hili, wanamdhihaki, wanawadanganya wananchi, au limewekwa kwa lengo gani? Maana Rais Magufuli, kwa hakika ni kinyume kabisa cha Unyenyekevu, na wala hata yeye haipendi hiyo tabia ya unyenyekevu. Watanzania tuache unafiki, tumwelezee mtu katika uhalisia wake.
 
Ni kweli kabisa. Kwanza anapenda sana kuabudiwa. Awamu zote hakujawahi kutokea rais anayependa kuabudiwa kama huyu. Akiwa kwenye mkutano akimtaja mtu, huyo mtu ni lazima asimame na kuinama kwa heshima. Mbona awamu nyingine haikuwa hivyo?

Kila kitu anapenda asifiwe ni yeye anafanya. Kwenye awamu hii ndiyo misemo kama ''ikikupendeza mheshimiwa rais... tunaomba.....'' Kwa kifupi amejikweza na kujiweka juu mawinguni. Anafikia hatua ya kufokea wafanyakazi na kuwaambia... ''yaani mimi ndiyo unanijibu hivyo.....''.
 
Mbele ya kura baba yake kula, kila mtu hupenda kuitwa mnyenyekevu na kila chama hupenda kiongozi wao aonekane mnyenyekevu vinginevyo hakuna kula bin kura.
Si lazima kila mmoja awe na sifa zote nzuri. Hata kama walitaka kumwinua mgombea, wangetafuta angalao sifa anazoshabihiana nazo.

Ni sawa, leo hii, atokee mtu aseme, Tundu Lisu ni mkimya. Wote tutashangaa, hata yeye Lisu atashangaa.

Kuwepo kwa bango ambalo ni kinyume kabisa na tabia zako - mgombea mwenyewe hashtuki?
 
Na wewe unaongea bila hata kutuonyesha kizibiti
 
Ndugu yangu Bams, naona umesahau kuorodhesha sifa zake hizi...
  1. Ni kiongozi katili
  2. Ni kiongozi anayekurupuka
  3. Ni kiongozi asiye na hekima
Nilimalizia kwa kusema kuwa, 'anaweza kuwa na sifa nyingine lakini tusiwe na uthibitisho wa moja kwa moja'.

Kwenye ukatili, nadhani ushahidi wa wazi upo. Kuwabomolea nyumba watu ambao hujui watalala wapi, kutumia michango ya wahanga wa tetemeko kwa mambo mengine na siyo ya kuwasaidia wahanga moja kwa moja.

Kukosa hekima, nakubaliana nawe. Kwenda kuwasimanga watu waliopatwa na tetemeko, eti ukimwi umeanzia kwao, vita ya amini ni wao, na sasa tetemeko kwao, n.k. Yale siyo maneno ya kiongozi mwenye hekima kwa watu wanaoomboleza. Asante kwa kuongeza hizi sifa nyingine zenye uthibitisho wa wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna bango moja la mgombea wa kiti cha Urais, Mh. Magufuli linasema eti Magufuli ni mnyenyekevu!

Nilipoliona bango hili, nikashtuka sana. Nikajiuliza maswali mengi:

1) Ni Magufuli mwenyewe amehiari kuwepo kwa bango la namna hiyo?...
Awe mnyenyekevu kwa kila kitu ili mpige dili vizuri.?
 
Bams umesahau pia sifa yake kuu ya uongo. Mfano halisi ni huu mwenendo wa kupika data ili kuonyesha hali nzuri kinyume na ukweli. Jaribu kuangalia idadi ya wapiga kura, inasemekana wapiga kura ni 29m+, huku raia wa Tanzania tukiwa 59m+.

Inawezekana vipi watu wazima yaani 18yrs+ kwenye nchi, idadi yao ikawa sawa sawa na walio chini ya umri huo? Kwa idadi hii ya kupika ina maana kila raia wawili wa Tanzania mmoja kajiandikisha kupiga kura. Idadi hii ya uongo ya wapiga kura, ni maelekezo yake, na mtu muongo hawezi kuwa mnyenyekevu.
 
Kuna bango moja la mgombea wa kiti cha Urais, Mh. Magufuli linasema eti Magufuli ni mnyenyekevu!

Nilipoliona bango hili, nikashtuka sana. Nikajiuliza maswali mengi:

1) Ni Magufuli mwenyewe amehiari kuwepo kwa bango la namna hiyo?...

Nimewaambia ndugu zangu kama 30 hivi kwamba wakichagua ccm wasije wakaniambia wana tatizo lolote nikalitatua. Na uzuri wamenielewa baada ya kuwapa darasa la nguvu.

Nashauri wagombea wa ccm waache kubeba watu kwa malori alafu tuweke uwiano nani anajaza watu kwa hoja na wasiwepo wasanii kwenye majukwaa
 
Mbele ya kura baba yake kula, kila mtu hupenda kuitwa mnyenyekevu na kila chama hupenda kiongozi wao aonekane mnyenyekevu vinginevyo hakuna kula bin kura.
Safiii
 
Mtu aliyewavunjia wananchi nyumba bila huruma, akakataa kusaidia watakaokumbwa na baa la njaa, akapora haki ya uchaguzi ya wananchi kwenye serikali za mitaa, akakataa uchunguza matukio ya wasiojulikana, akateua mafisadi na akawapa nafasi za kimamlaka, akafunga watu jela kwa uonevu, akanyanyasa wapinzani, akanunua wapinzani njaa na kuitisha chaguzi za kimagumashi na kuwashindisha kinguvu aliowanunua, akatumia nguvu za kijeshi kutwaa korosho za wananchi

Huyu ndo mnyenyekevu huyu?
Acheni kutania Watanzania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…