Bank ipi ni bora for saving na makato yake ni nafuu

Usiporidhika na michango waliotoa wengine, jaribu kuweka kwenye VODA M-PESA!
 
Benki zote ni hovyo kabisa ila sasa kwenye huo uhovyo kuna wenye uhovyo afadhari na uhovyo sana. Cha msingi benki bomu kuliko zote ni NMB, ila kama maisha yako yatakuwa ni ya vijijini huna ujanja maana ndio benki pekee inayopatikana mpaka vijijini. Benki inayofuatia kwa uhovyo ni NBC, hawana tofauti kubwa na NMB, foleni ni ndefu mno, kama una muda wa kuchezea wa kukaa benki masaa manne mpaka nane unaweza ukaopt hizo benki mbili. Benki zingine customer care yao ni hovyo sana kama vile wamelazimishwa kufanya kazi. Ila kwa benki ambayo ni hovyo afadhari ni CRDB, wanajitahidi kuendana na wingi wa wateja wao maana wana mabranch mengi, so ukiona branch moja mizingua unaweza enda branch nyingine, ila km kuna tatizo lolote utakalopata linalohusiana na Card yako, inabidi usubiri mwezi kuweza kurekebishiwa tatizo.

Barclays ni benki hovyo sana japo pia inajitahidi kuwa na branch nyingi, unaweza ingia bank mkawa watu 6 tu ila utasubiri hapo masaa mawili, huku wakitoa majibu mepesi tu kuwa system ipo slow au down, watu hawajitumi kabisa, unaweza ukakuta foleni ndefu halafu bank teller mmoja, wengine wanapiga story tu. Kadi zao hazina picha, so ili ufanye transaction ni lazima uwe na kitambulisho kingine, pia wizi mkubwa waliofanya wafanyakazi wao wakati wanatoa mikopo kiholela umesababisha wawe na kero nyingi zaidi kwa wateja wao.

Benki zingine zote ni matatizo tu, zina branch chache sana hapa nchini. Kwa ujumla ukiamua kuweka hela zako bank inabidi uwe na moyo wa uvumilivu.
 

Mkuu hapo umenena kabisaaa, mi nakumbuka one day nilienda kupokea hela kwa western Union, katika zile hela kulikuwa na noti moja ya 2000 ilikuwa imechakaa mbaya sijapata ona, nikamuomba anibadilishie akasema hamna wakati naziona note zipo pale counter. Nikamwambia kuwa Bank moja ya kazi zake sio kusambaza noti zilizochakaa, alinijia juu na kusema hanibadilishii na ataona ntafanya nini.., nikawa mpole. Nilikuwa nna kadi yao nilichofanya ni kuwithdraw hela zangu zote next day na kuichoma kadi yao. Yaani sitaki hata kuwasikia:rip::rip:
 
vipi kuhusu standard chartered, sijasikia maoni kuihusu? kuna yeyote mwenye experience nayo?
 
bank nzuri bongo ni kununua ardhi thn siku unataka kudraw unaipata hela yako kwa riba ya up to more than 100%, ila hela ya kula kuwa nayo nyumbani kwako, ya kuhifadhi ndo kununua ardhi, it has worked for me alot, bongo hakuna bank ni upuuzi mtupu!
 
vipi kuhusu standard chartered, sijasikia maoni kuihusu? kuna yeyote mwenye experience nayo?

expensive kurun account, wnakukopesha kwa lazima ukishindwa lipa wanakusumbua sana sana, na vitisho kibao,
 
Pita katika bank zifuatazo uone offer zao, hapa kila mtu atakwambia lake: Shortlist yangu in terms of reliability na costs: Standard Chattered wana product mbili nzuri Tajirika account ambayo unapata profit kwa deposit ya 50,000 na kiwango cha chini kinachoendelea kukua ni 10,000; na savings account yenye ATM na cheque book bila makato ya Mwezi ila ukidraw ndo wanalamba 500 kama kawa. CRDB in terms of capital na security pia service zao zinaimprove everyday. Barclays kwa maswala ya mikopo n.k.
 
Kibubu ndiyo dawa.............mabenki makato yao makubwa sana...............banking is business....business is all about profit
 
Kibubu ndiyo dawa.............mabenki makato yao makubwa sana...............banking is business....business is all about profit
Hahahaha tatizo la kibubu wanaweka Chuma Ulete
 
Habari zenu wana jf
ningependa kujua bank ambayo ni nzuri kufungua kwa mwananchi wa kipato cha kawaida
kwa kuzingatia vigezo kama
-makato kwa mwezi
-kianzio cha kufungua account
-huduma bora kwa wateja
-mikopo ya riba nafuu
-kuenea kwake nchini
nawasilisha
 
Hiyo point ya mwisho ni muhimu sana kabla hujashauriwa. Unaishi wapi mkuu? Maana bank zingine ni nzuri lkn zinaweza kuwa hazipo unapoishi
 
kwakuwa wewe ni al shabaab islamic bank itakufaa sana na hakuna mambo ya riba kule.
 

Mpesa ....

-Unaweka na kutoa pesa wakati wowote.
-Unatuma na kupokea pesa (m-powa) muda wowote.
- Haina foleni.
- Kukopesha na kukopa
- Imeenea nchi nzima
........,..,.............,
 
...nbc is the best,ingawa wako slow lakini wako makini sanaaa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…