Bank kutoza "processing fee" kwenye mikopo ni uwizi mkubwa.

Black Legend

Senior Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
174
Reaction score
301
Kumekuwa na mfumo huu kandamizi wa bank nyingi Tanzania kumtoza ada ya kupitisha mkopo mteja wa bank hizo. Ukiangalia kiundani,kuandaa mkopo na kumhudumia mteja ni jukumu la bank.....mteja aishie kukatwa riba tu na sio vipengele vingine kandamizi kwa mteja.
 
NI bank karibia zote zina huo mfumo
 
Hapo unachotaka ni riba ipande sababu zile ni gharama nyingine zisizohusisha muombaji mkopo kukodishiwa fedha kwa riba.
 
NI bank karibia zote zina huo mfumo
Zile ni one time payment boss. Hata mm huwa zinanikera sababu zinaongeza gharama ya mkopo tatizo ni kuwa wakizifuta zile hii gharama uwezekano ni mkubwa mno itaamia kwenye instalment fee na kuongeza tatizo la riba unless BOT ihakikishe gharama aihami.
 
Unaweza nipa m hanganuo wa hiyo "processing fee" mkuu?
Mara nyingi ukiuliza watakwambia ni paperwork, gharama ya uhakiki dhamana, kutembelewa n.k.

Yaani zile gharama za uhakiki kuwa unakopesheka.

Huwa sioni kama ni gharama ambazo mkopaji anatakiwa kulipia, ni sawa na uende dukani mwenye duka akucharge gharama za daftari la kuandikia mauzo yake ila sasa tatizo ni wakizifuta zinaamia wapi?

Maana hayo ni mapato kwao na tunajua yapo pale kihalali na yamekubaliwa na BOT ili mabank wasitegemee riba tu, ukifuta uwezekano ni wataziamishia kwenye riba, sasa kuliko hivyo bora zibaki hapo au BOT wawe serious na hilo haswa.
 
Kumekuwa na mfumo huu kandamizi wa bank nyingi Tanzania kumtoza ada ya kupitisha mkopo mteja wa bank hizo. Ukiangalia kiundani,kuandaa mkopo na kumhudumia mteja ni jukumu la bank.....mteja aishie kukatwa riba tu na sio vipengele vingine kandamizi kwa mteja.
Hakika ni wizi mkubwa.
 
BOT hua wanasimamia Mambo gani hivi
 
Yeees ,hapa nadhani tumeelewana. Tunalipia majukumu yao ya kutoa huduma unayoilipia. Uende dukani halafu mwenye duka akutoze Hela ya kutoa bidhaa kwenye shelfu za duka......hii ndio nimeandika kuwa ni WIZI .🙏🏼😡
Huo ni uwizi BOT sijui wanasimamia Mambo gani nchi hii
 
Bankers wanaishi ki executive, wakopqji wanaish kama Manyani..

Mikopo aina nyingi inayotolewq na Bank hai make sense, maipende kukopa kopa ikiwa hauna financial literacy
 
Kumekuwa na mfumo huu kandamizi wa bank nyingi Tanzania kumtoza ada ya kupitisha mkopo mteja wa bank hizo. Ukiangalia kiundani,kuandaa mkopo na kumhudumia mteja ni jukumu la bank.....mteja aishie kukatwa riba tu na sio vipengele vingine kandamizi kwa mteja.
Najiuliza sana kwanini BOT waliruhusu kitu kama hiki. Hakina logic kabisa zaidi ya wizi wa waziwazi
 
Mara nyingi ukiuliza watakwambia ni paperwork, gharama ya uhakiki dhamana, kutembelewa n.k.

Yaani zile gharama za uhakiki kuwa unakopesheka.

Huwa sioni kama ni gharama ambazo mkopaji anatakiwa kulipia, ni sawa na uende dukani mwenye duka akucharge gharama za daftari la kuandikia mauzo yake ila sasa tatizo ni wakizifuta zinaamia wapi?

Maana hayo ni mapato kwao na tunajua yapo pale kihalali na yamekubaliwa na BOT ili mabank wasitegemee riba tu, ukifuta uwezekano ni wataziamishia kwenye riba, sasa kuliko hivyo bora zibaki hapo au BOT wawe serious na hilo haswa.
Hawatakiwi kuzihamishia popote, ule ni wizi tu! Mimi nadhani ziliwekwa zamani sana ambapo benki ilikuwa moja tu na hapakuwa na ushindani hivyo badala ya mkopaji kuonekana mteja alionekana kama muomba huduma ndiomaana walimchaji vyote hivyo.

Sekta ya benki imeshakuwa hizo gharama BOT inabidi izifute.

Hivi wanafunzi wa sheria wanasoma nini mashuleni huko? Maeneo ya kufanyia practice ni pamoja na kufungua kesi kama za kufuta sheria kandamizi kama hizi
 
Nilipomsikia Madilu Bungeni Anaulizwa Na Speaker Kuhusu Riba Kubwa Akajibu Ni Soko Na Hupangwa Kulingana Na Hali Ya Wakati Huo Ipoje
Nikaona Kumbe BOT, WIZARA YA Fedha Hazina Msaada Wowote Unapokopa

Benki Na Mikopo Yao Siyo Rafiki Wa Masikini Kamwe. Kausha Damu Zimejaa Kwenye Benki
 
Back
Top Bottom