Bank tellers na "udokozi"

Consultant

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2008
Posts
11,503
Reaction score
20,892
Jumamosi nilienda KCB branch moja Posta na kuchukua 4.5M. Yule teller akanipa zile bundles za buku tanotano. Sikumtilia shaka kutaka azipitishe kwenye mashine maana alionekana kama "muungwana na mstarabu" flani hivi na nilikuwa na haraka kidogo. Jana nazihesabu na kukukuta kumbe alinipiga jumla ya Tshs. 45,000/=.

Be warned. Siku ukiona teller yeyote hataki kupitisha mpunga kwenye machine, shtuka. Ni bora uonekane mbishi na upoteze muda wako kidogo kuliko kujuta baadae
 
Kwani 45000 mbona sio kubwa kama million 4.5. Ulishindwaa hata kupima kwa macho mzee, au ndo kutaka kutudanganya
 
Duh nikiwa mdogo enzi hizo elfu kumi ni hela haswa nilipeleka fedha za mauzo CRDB hakika nilitoka na vidonda vya moyo havijakauka mpaka wa leo. Dada mmoja sura yake imenikaa kichwani sijui lini nitaisahau.

Nimetoa fedha mafungu kama matatu niliyoyahesabu kwa unakini wakati natoka nyumbani na kurudiwa na mlezi wangu mbogo kuliko mbogo. Kumpa dada wa benki ananiambia elfu ishirini imepelea akanirudishia fedha nihesabu mwenyewe tena.

Niliziacha hapo nikaenda kukaa kwanza mapigo ya moyo yakienda mbio hatari nikitafakari namna ya kukutana uso kwa uso na yule mbogo kule nyumbani huku nikieleza kilichonisibu.

Kumbe dada yule alizidondosha chini makusudi fedha zile. Sikudeposit tenanikarejesha fedha nyumbani kilichonikuta Mungu pekee ndiye anaweza kukisamehe..
 
mtoa mada upo vizuri sana naona sekeseke la uchumi halijakukumba yani hutoe hela jumamosi ukae nazo bila mishe yoyote hadi j4 ulienda kuzificha nini! afukama umetoa hela jumamosi unazihesabu jana sikuzote zilikuwa wapi? je kama mkeo au watu wakaribu wamenyofoa?
 
Pole sana. Mie pia nimewahi kufanyiwa hivyo na bank teller wa CRDB Lumumba
 
Sio kuficha mkuu. Kuna watu nilitaka kuwalipa wakazingua kazi nikaahirisha. Mpunga haukuguswa na yeyote maana niliuweka sehemu salama
 
Pole sana. Mie pia nimewahi kufanyiwa hivyo na bank teller wa CRDB Lumumba
Hatari sana hii. Inasemekana pia baadhi ya tellers wa CRDB ndo mchezo wao huu. Hali ni ngumu ila udokozi kwa style hii haukubaliki.
 
Wakati anazichomoa wewe ulikuwa wapi
 
hiyo tabia inakera sana, tatizo hata mabenki yakipeleka pesa BoT kudeposit huwa wanaambiwa pesa zimepungua, sifikirii kama imewahi kutokea wakaambiwa pesa zimezidi.
 
Natamani uendelee kusimulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…