Bank yenye riba nafuu

Nyam

Senior Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
134
Reaction score
72
Habari wana jf, mimi ni mdau wa hili jukwaa na huwa linanisaidia sana..Leo ningependa kufaham Bank yenye riba nafuu mbali na NMB kwa sababu NMB nina deni ambalo bado halijaisha naendelea kulitumikia..Mimi kwa sasa nafanyakazi kwenye kampuni binafsi hapa Dar,nataka mwaka huu kabla haujaisha niwe nimenunua kiwanja angalau cha mil.3 ili niweze kutimiza ndoto zangu, kwa iyo ningependa kujua bank yenye riba nafuu ambayo nitaweza kukopa 3mil na makato yake yawe kuanzia miaka 3 na kuendelea...
 

Mkopo wa m3 uulipe kwa 3 yrs? Na huo mkopo nmb uliufanyia kaZi gani
 
Nataka uwe wa miaka 3 ili makato yangu kwa mwezi yasiniumize yawe madogo...Mkopo niliochukua NMB na wenyewe ulikuwa ni wa miaka 3 kiasi hichohicho cha 3mil na unaisha mwakani mwezi kama huu..Mkopo wa NMB nilimpeleka mama angu India kwa ajili ya matibabu na namshukuru Mungu anaendelea vizuri..
 

Benki nyingi Riba zao ni kati ya 18-25 kwa watu wakawaida. Inakuwa pungufu ya hapo kwa taasisi au makampuni. Sababu ya riba wanasema ni risk kwa watanzania hatukopesheki na hatuaminiki. Kwa matajiri wakubwa kama akina Rostam na SACOS wanakopeshwa kwa riba hafi 3%.

Ushauri wangu jiunge na SACOS za kidini hasa za makanisa zitakutoa umasikini.
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako ngoja nkajaribu kuulizia kanisani kwetu Katoliki hapa Kinondoni kama watakuwa na SACCOS ili nijiunge...
 
Bayport hata mimi sikushauri.... CRDB riba ya makampuni binafsi ni 20%..... KCB ni 21% kama sikosei... Ila nadhani its best ukifanya personal survey katika mabenki husika utapata taarifa za uhakika zaidi...
 
To advise, save from your salary or any means of income you currently have. RIBA is religiously prohibited whether you're Christian or Muslim (I suspect you're within one of these two). Go for NBC Malengo account or any other bank (they all have this kind of account) to start saving.

Shortcut ndo inawaumiza watu, capital inatafutwa jamani. Usije ukajirusha ghorofani wenyewe wanapokuja kuchukua vyao....

Say no to devil :shetani::shetani::shetani:
 

SACCOS zinaweza kulipisha riba kama ya kiasi gani?? Maximum wanakopesha kiasi gani?
 
Nenda Abc bank kwa kiwango hicho na muda huo,utakatwa 148,616 pia ukitaka kulipiwa deni lako pia inawezekana.
 
ABC Bank Tanzania
 
Cku moja nilisikia kwenye taarifa ya habari benki moja inajiita ya kiislam hawatoi riba kabisa kwao ni dhambi hawabagui wateja.Hebu jaribu kuwaona na kuulizia huko huenda ukafanikiwa.

Inajiita?! Hapakuwa na sababu ya kutumia hilo neno..!
 
Riba maximum 10%. Kiasi cha mkopo maximum ni akiba yako x3. Mfano umeweka akiba 10m unaweza kopa 30m. Kiukweli sacos ni mkombozi kwa mtazamo Wang.

Basi hainifai, utawekaje milion 10 sehemu?? Badala ya kuizungusha ilete faida?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…