Bankers wanahitajika..

hahahaaaa Mopalmo,usiogope mapimbi huwa wapo kila siku,lakini kama ulitumia njia flani ukafanikisha kupata kazi,waambie na wenzio,tatizo siku hz watu wanafikiri kila aliyepata kazi alitoa pesa
..so anaona ukiweka tangazo humu unataka kutapeli watu...huu ni ufupi wa mawazo..
 
Kama kuna mtu atahitaji bado kutumia ile email address pale juu,atume,kiroho safi nita i forward kwa HR,kama huamini kama wenzio,basi njoo mwenyewe hapa mjengoni......

mi huwa nawashangaa sana watu, kuna thread nilianzisha hapa kuwaambia watu watuambie experience zao kuhusu ATM zetu za umojaswitch, nilikua nataka kupana maoni na pia kupata kero wanazokutana nazo wateja.

kuna watu wakasema, huyu ni tapeli la ki-nigeria, uoga wa hivi nao ni ujinga, mfano, your financial institution is not available, what does this msg mean? nitakuibiaje? nakuambie niulize mimi ntakupa info wewe unasema nataka kukuibia, how?

inafanana na hii issue, tuma application, unaibiwaje hapo? hebu tuwe tunafikiri, msiwe wepesi hivyo!
 
Kwa heshima na taadhima naomba nimsaidie Majany! Sasa hivi nimepiga simu 022-2863458 na wamenieleza kuwa ni nafasi moja imechukuliwa. NASHUHUDIA kuwa ni ukweli tupu nyie akina kaka.

nimekupenda bumukunda!
 

Hivi unajua CV yako inahold vitu gani? Unadhani ni kwanini makampuni yanatoa kiapo kuwa hawata disclose viambatanishi na CV yako elsewhere bila consent yako. Mkuu suala la kutuma CV na viambatanishi kiholela usizoeee hata kidogo.

Usije ukashangaa naajiriwa kwa jina lako ww Uswe
 

huyo muajiri atayetoa ajira bila kumthibitisha mtu anayetaka kumuajiri nisingependa kufanya nae kazi, hapa unamaanisha akipata tu cv na copies ya vyeti hata kuona originals, hataki kupata references nk siyo?

mwajiri wa hivyo hayuko makini na nisingetamani kufanya nae kazi. . . atanisumbua!
 
Owkey...nazidi kuondoa utata,nimempa Hr hiyo e-mail adress pamoja na password yake,kwa hiyo ukituma,itamfikia moja kwa moja bila kupitia kwangu,ni kwa nia njema tu,ili wadau kama BIO-HAZARD povu liwaishe na waendelee kuchapa kazi ili kupiga jeki maendeleo yao na familia zao...

BIO HAZARD weeee.....usidanganye umma kwa woga wako,naamini huna C.V nzuri kiasi cha kunifanya niamini kila mtu ni threat kwako,kuna watu wana C.V nzuri kupindukia,na still wanaziweka online,uki 'GOOGLE' unazipata.....usitudanganye wewe....
Nimesoma UDSM,ukiingia ARIS unapata C.V za walimu woote,hata HAROUB OTHMAN(R.I.P) ambaye naamini humkuti hata kwa theluthi aliweka hadharani CV yake......wewe utakua magamba,ndiyo huficha C.V zao,kwa kuwa zimejaa maurongoooo......
 
nimeweka kila kitu kwenye thread,soma na utiririke
 

Mkuu mie sina CV nzuri ila nina MKATABA MZURI pia nina BIASHARA NZURI ukishoboka na CV hapa mjini utakula maneno yako.

Yeye alianika CV yake kwa kuridhia mwenyewe. Kingine unapoamua kuwa Mbunge au Mhadhiri na kwinginepo kuna terms lazima uzikubali ndipo wanaweka CV yako ina maana ukikataa huna kazi.

Mfano Profile ya Chuo lazima wahadhiri wake waweke CV pamoja na Bunge pia baadhi ya makampuni wanafanya hiyo kitu kwenye profile zao ili kuongeza trust.

Mkuu kwa taarifa yako ww kidarasa nina rekodi nzuri nikianza kusema mie TO ndio kuonekana kama kina Mwigulu wale wa uchumi daraja la kwanza.
 

Mkuu hapa mjini hao waajiri ni wengi sana mtu anakuja na vyeti tena Certified huku akilia aliibiwa begi la laptop na vyeti vyote hapo alipo anafanya mpango wa kutangaza kwenye gazeti ontop of that anapigwa intervew anaonekana ni potential mbona wamechukuliwa wengi sana mkuu kwa hizo staili.
 
Tapeli ww Taasisi ya kifedha haiwezi kutumia Live domain mkuu. Kwaibie Facebook huko. Labda ungheandika email ni recruit@[COLOR=#b22222]ubagroup[/COLOR].com

Kwenda Zako huko




mkuu biohazard advert umeiona???waweza kutuma pia kama unaona unafit...


sihitaji hata kumi yako....kama umeona vigezo vimekutupa nje kaa kimya ili waliokua serious shuleni wachukue kazi..pimbi..wewe....umeombwa utoe kipi???povu lukuki




Kwanza nawaomba radhi wakuu wote niliowakwaza

Wakuu wote napenda kuchukua nafasi hii kuwahakikishia kwamba kazi alizopost huyu ndugu yetu ni kweli zipo pia nimeongea na HR wa pale UBA ameniambia wamekuwa wakiwatumia RADAR kama recruitment Agent wao lakini kwa sababu zisizozuilika wameamua kurelease hizo kazi wenyewe na mnaweza kuomba bila shaka lolote.

Ushauri:
Ndugu zangu mnaopost humu ndani msijaribu kuwekaweka emails ambazo sio za makampuni husika na hili ndilo tatizo ambalo linfanya watu tuwashuku kua ni matapeli. Am so sory majany bila kumsahau Uswe

Nawatakia mafanikio katika maombi yenu ya kazi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu asante bwana ngoja nitume cv hiyo!!kitaa kumeshanichosha sana2
 

You did not do anything wrong, ulikuwa unataka tu watu wapate correct information na sio magumashi.
 
You did not do anything wrong, ulikuwa unataka tu watu wapate correct information na sio magumashi.

Sawa sawa mkuu maanake hapa mjini watu wengi wanasumbuliwa na hili wingu la matapeli wa ajira sana. Mie nimeona nilifuatilie kwa kina zaidi sababu ndugu yetu hakuchoka kutuhakikishia kwamba hii kitu sio chogi bali ni kweli. Na inaonekana hawa jamaa wanataka watu kweli kwenye hiyo fani na wengi tunao apply tumeshindwa kufikia vigezo.
 
Watu wanapenda kuchonga sana, hivi mnadanganywa mara ngapi, maboyfriend, nyumba ndogo tena kwa vitu visivyo na maana. Kama huna shida na kazi ukikaa kimya utakufa?

Ona sasa! aibu! lol
 

Kwa nini hukufanya uchunguzi kwanza ndio uongee?? unakuwa kama serikali ya Tz.....kukurupuka tu...wakija wakijua ukweli huwa wanakuwa wadogo kama Priton....
 

Tatizo ni kwamba hukutaka kusikiliza utetezi wake. majany alishazungumza mapema kwamba lile tangazo ni internal advertisement....kwa kawaida, internal advertisement ni maalumu kwa wafanyakazi wenyewe na labda, akikosekana mtu miongoni mwao; huwa wanapigiana mapande ndugu kwa ndugu!! alichofanya majany, ni kutoa mchongo kwa members wa JF....mimi siamini kwamba katika dunia hii kuna graduate ambae anaweza kukosa ndugu ama washikaji wa kuambia kwamba kuna mchongo mahali....! Hata hivyo, badala ya kuwaambia washikaji peke yake, majany akaamua kutushirikisha hata hakina sie tusiejuana nae.

Na hilo la kutumia domain ambayo sio ndiyo, u may have a point; lakini usikariri! Na kama alivyosema majany, baadhi ya email domain za baadhi ya makampuni, huwa haziruhusu email kutoka nje. Hata mimi, kuna sehemu nilikuwa nafanya kazi....any outside email, haiwezi kuingia through email address ya hiyo kampuni. Ni jambo la kawaida sana hilo....hususani kwa mabenki!

All in all, big respect for your apology!
 
Noted..kiroho saafi kabisa,kama ulivyosema wengi wetu hatu'meet vigezo,na wewe pia BIOHAZARD,peleka ujumbe huu wa kazi kwa colleague wengi kadri uwezavyo..Nawahakikishia,UBA hakuna cha rushwa wala nini,ukionyesha unaweza,lazima uchukue kitengo.Pia,believe me,UBA iko above average kati ya benki nyingi tuu interms of payment....
 

Karibu na hongera kwa kuwa muungwana, common sense ilikua inasema hakuna wizi wowote kwa hili, nilikuasioni ni vipi mtoa mada anaweza kukutapei kwa mazingira haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…