Banki sio rafiki kwa Mfanyakazi/mtu wa kipato Kidogo

Naona mmekuja kujipa promo 😣😣 hamnipati nyie
 
Ulaya mortgage ndio mkombozi wao.
Nashukuru kwa mchango wako. Kumbuka kwa nchi kama England. Kupata nyumba ya vyumba 3 ambayo ina kila kitu na sebure, jiko, kistooo kidogo na ipo nje ya mji na ghorofani juuu uko kama ya 14 na kuendelea inachezea 400~600Milioni ya Tanzania. Na ndio maaana wenzetu wamewekeza ktk kupanga hana shida ya kununua nyumba kwa sababu gharama ya maisha yake akipiga maesabu ana shida ya kumiliki nyumba anaona kero maswala ya kodi, kuwa karibu na serikali incase umempangisha mtu akaleta ishu kama za ughaidi. Kwa wennzetu wapo makini sana
 
ktk faida angalia na muda, kumbukuka 2006 ni miaka 13 iliyopita, wakati huo canter tone 3 narobo, zilikua million 8 sasa hivi ni zaidi ya million 20.
 
ni kweli, tulikua tunatumia roller tatu, na mota hp 40, na ya kusaga hp 30
Kama ulikuwa unatumia roller tatu Kwa hp 40 lazima umeme ukule pia usikute mota zenye zilikuwa za kusukwa. Kwa roller tatu kumaliza tan kumi no mtihan lakin Kwa roller tano kumaliza tan kumi Kwa masaa 12 no kugusa Tu. Kwangu Mimi mashine tunazouziwa na Sido sijui milion tatu naona kama wanatula.
Mfano mdogo Tu nikisema ninunue vifaa mwenyewe Kwa mashine ya kukoboa Kwa mashine ya roller tano
Shaft 270000
Roller tano 100000
Flat bar Kwa 24000
Bat zito 80000
Chekeche(5)@6000= 30000
Pulley inch 8 = 60000
Mfuniko = 200000
Ufundi na vifaa vyangu kuchomelea 500000
Mpaka hapo nachomoa mashine ya roller tano Kwa pungufu ya million moja na laki nane lakini roller tatu utauziwa million tatu na mota ya hp 30 ambayo Kwa ujumla inafaa kusagia watu wa rejareja Ila sio Kwa heavy duty
 
ktk faida angalia na muda, kumbukuka 2006 ni miaka 13 iliyopita, wakati huo canter tone 3 narobo, zilikua million 8 sasa hivi ni zaidi ya million 20.
Hata SAA hii tani kumi haifiki milion Saba dar na hizo tani thelathin no pungufu ya 20mil, labda uwe unazungumzia arusha huko Ila Kwa dar bado mahindi kilo haijafika 700.
 
Hata SAA hii tani kumi haifiki milion Saba dar na hizo tani thelathin no pungufu ya 20mil, labda uwe unazungumzia arusha huko Ila Kwa dar bado mahindi kilo haijafika 700.
hapa hujanielewa, nilikuwa nazungumzia thamani ya Pesa. mfano niliotoa ni wa kununua gari, aina ya canter, wakati huo ilikua unaagiza kwa million 8, lkn kwa sasa inazidi million 20.
 
Pengine wanakopa ili wajenge nyumba za biashara
hapana mkuu.

wanakopa wananunua uwanja na kuweka foundation ndani ya miezi mi3 mkopo umeisha na kiwanja kipo foundation.

hapo atadubiri miaka mitatu au minnr ipite akakope trna ili apandishe tofali.

then analalamika mshahara mdogo kila akikaa na watu analeta story hixo tu(sina maana mshahara usipande)
 
Huo mkopo sio wa kwenda Bank. Ndugu zako 2 tu wanaweza kupa hio na ukarudisha bila riba. Shida wengi hamuaminiki. Nilimpa jamaa bodaboda aendeshe arudishe tu nusu ya hela (mdogo wangu) hadi leo sijamsikia nimeamua kukaa kimya.
Yaani ndugu wakupe 2.5M mkuu bilashaka unatokea familia zakina MO wewe....kwa ukiri yako angeenda Bank kama ndugu wanaweza mpa.
 
Mkuu nimeona nami nitie neno hapa kwani mchanganuo wako hapa janvini nimeupenda ila mimi ni mtu wa rejareja nataka kuwin soko la usagaji hapa nilipo kwa kuboresha quality ya unga naosaga kwenye mashine yangu ila kuna mtu alinishauri nichukue kinu cha size 75 na motor 30Hp ndio itatoa unga kama ule kama wa supplier wengine ambao mashine zao ziko kibihashara naamanisha wanasaga na kupaki kwani wengi wanaonizunguka wanatumia 20Hp na 25Hp na vinu vya saizi 50,

Je unga utaotoka kwa kutumia hizo motor 30Hp na kinu size 75 utaweza ku-meet my expecation?
 
Kwa muono wangu unga mzuri unaanzia kwenye ukoboaji. Mara nyingi naweza kusema ukiwa na mashine ya roller kuanzia tano na ukayabana vizuri mahindi ukija kwenye usagaji no ishu ya chekeche. Kwangu Mimi chekecheo nayotumia ni moja na robo,
Tukija kuwa supplier mkubwa kitu tusichojua Kwa mashine ya size 50 au 75 na mashine ya kukoboa ya roller tatu sitarajii kama utaweza timiza malengo kihaswa maana ili utengenezaji pesa inabid uzalishe Kwa wingi uuze bei ya wastan huku ukipunguza gharama za wafanyakazi.
Kwa ushauri chonga mashine ya kukoboa roller tano mota hp 50 mpya hata za kichina Ila za rpm 1440 na mashine oversize ya kusaga kama unaweza nunua plate mwenyewe kama inchi 12 tafuta fundi akutengenezee. Ukiwa na mashine imara hata ukija weka pulley mfano kwenye mota inch 12 Kwa inchi 3 Kwa mashine utanambia moto wake. Kuna watu nasikia wanafunga mpaka gearbox ili kupunguza ulaji umeme sijawahi kutana na technolojia.
 
Inaonekana hii biashara ukitulia unaweza piga hela ya maana. Mtaji unaweza kuwa kama kiasi gani kwa mtu ambaye anaanza from scratch?
 
Inaonekana hii biashara ukitulia unaweza piga hela ya maana. Mtaji unaweza kuwa kama kiasi gani kwa mtu ambaye anaanza from scratch?
Inategemeana na eneo. Kuna sehem ukishasimika mashine na mahindi unapata hata Kwa mkopo unabaki kupambana na soko.
Kiujumla hii ni biashara kama biashara nyingine kuna ugumu wake pia kinachohitajika ni determination.
Minimum ukitaka uanze vizur ni kama 15mil pamoja na mashine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…