Banki sio rafiki kwa Mfanyakazi/mtu wa kipato Kidogo

Banki sio rafiki kwa Mfanyakazi/mtu wa kipato Kidogo

Yqonekana hujawahi fanya biashara wewe..


Hiyo saving mpaka ifike 5m ingekuwa rahisi si kila mtu angesave....


Unaijua maana ya riba???
Na kwa nini kuna riba??
lengo la riba ni mkopeshaji apate faida baasi.

usitake kuleta mengine
 
Lakini pia hiyo biashara inatakiwa uwe tayar ushaianzisha na umeona utokaji wake. Siyo umeifikiria tu kichwani then unaenda kukopa. Wengi wameumia sana.
Mikopo ni kwa ajili ya biashara. Sio unakopa kununua gari
 
Nimesoma hii thread nikacheka Sana.

Kwanza nianze kwa kusema mkopo wa fedha si tatizo Kama unavyojaribu kuelezea hapa ila tatizo ni mkopaji.Mkopo ni elimu kama ilivyo elimu nyingine ambayo inahitaji kujifunza na ku master the art of Dept.


Ili ufanikiwe una hitaji kujuwa namna ya kutumia kutumia pesa za watu wengine ambayo hawana kazi nayo(OPM) other people's money.Na hii ndo tunaita mkopo sio.
Sasa Basi lazima ujuwe kuwa anayekupa mkopo(bank) and the like,wao pale wanafanya Biashara na mkopo/fedha wanakupa ile ni bidhaa ambayo wao wanakuuzia hivyo wanatengeneza faida kupitia mkopo wao.Hii sio dhambi/vibaya Katika ulimwengu wa Biashara hii ni akili nzuri.
Mkopo kwa upande wa bank ni assets hivyo ita generate income in their assets colums.Pale hawakupi Bure ila wanafanya Biashara na wewe ( customer).
Sasa basi wewe mkopaji una wajibu wa kufanya mkopo kuwa assets or liabilities. Refer assets and Liabilities definition.
Assets are something puts that money in your pocket and Liabilities are something that takes money out of your pocket.Mkopo mzuri ni ule ambao unakopa alafu unaenda kuzalisha na kukuingizia pesa hivyo hautaweza kukumiza na kulipa kwa uchungu,ila mkopo mbaya ni ule ambao unaenda kukopa alafu unaenda kujenga/kununua liabilities ambazo zina kazi ya kutoa pesa na si kuingiza pesa.

My take:Unapotaka kuchukua mkopo lazima uwe na mipango thabiti ambayo itakussaidia wewe kulipa mkopo bila maumivu yoyote Yale.
Hapa sasa itakubidi uandae walipaji wa mkopo wako(tenants).Unaweza kukopa mkopo alafu ukajenga nyumba na ukapangisha means huo mkopo hautalipa wewe ila wapangaji wako watakuwa wanalipa mkopo wako bila wao kujuwa.
Wafanyakazi wengi ni wahanga wakubwa wa mikopo.
Loans is a leverage of getting rich
 
kukusaidia tu ndugu...ukichukua mkopo benki na kuulipa kwa mda mfupi riba inakuwa ndogo


mfano ukichukua milion 10 then uilipe kwa mwaka riba yake itakuwa ndogo sana kuliko atakaechukua hiyohiyo milioni 10 then ailipe kwa miaka 5

so huyo nduguyo hyo milion 100 kwa miezi sita ni sawa tu...ila angeilipa kwa miaka 5 isingekuwa milioni 6

Benki hawana hyo eti kisa ni mfanyabiashara Mkubwa basi upewe mkopo kwa riba ndogo hiyo NAKATAA..Benki ni taasisi ina taratibu zake
Kuna rafiki yangu ni mfanya biashara mkubwa kuna bank wamembembelezea pesa kinoma!
Kachukua mkopo wa milioni 100 kwa muda wa miezi 6,sasa cha kushangaza riba yake ni milioni 6 tu,wakati yeye pesa ameagiza contena ambalo hakosi faida ya milioni 20,ndani ya miezi sita shilingi itakuwa imezaa shilingi,Yaani anasema hadi miezi sita inakamilika atakuwa ashamaliza bank na mfukoni ana faida ya milioni 75,sasa utamwambia vipi mfanyabiashara asikope??
Bank wakiona ni mfanyabiashara mkubwa wanakupa pesa kwa riba Ndogo sana na bila masharti mengi tena kwa kukubembeleza!
Lakini wakiona huelewi chochote kuhusu biashara utapigwa riba hadi na za michepuko yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhh Kwa miaka 20 kiwango mbona kidogo sana.
Tuchukue update hizo milion 40 uwekeze mfano kwenye biashara ya utengenezaji wa unga wa sembe.
Kukodi jengo 300000*12'=3600000
Mashine ununuzi =8000000
Kuingiza umeme=2000000
Mifuko grade1 ya kuanzia(2000)=1000000
Mpaka hapo jumla=14600000
Unabaki na 25400000
Toa 25000000 kipind cha mavuno nunua Mahindra utapata kg 40000
TUJE KWENYE UZALISHAJI
Ukijiwekea target kila siku usage tani kumi Kwa wastan wa faida ya 300000 Kwa tani kumi. Hapa bila pumba.
Ukifanya Kwa siku 20 Kwa mwezi,
20*300000= utaingiza 6000000 Kwa mwezi.
Kwa mwaka 12*6000000=720000000
Kwa miaka 20*72000000=1.44bil
1.44bil-147mil=?

TUJE KWENYE DECISIONS
Kwa maono yangu tatizo sio benki Bali maono ya mtu na exposure.
Nipe Mimi hizo nikupe 200mil Kwa miaka miwili Ila au nipe machinery za that amount hiyo nichague eneo la kufanyiwa biashara nikupe mara kumi ya capital yako ndani ya mwaka.

Mifumo ya kibenk iko sahihi sana, changamoto iko kwa wateja. Ukichukua mkopo kisha ukaitumia kwenye matumizi yasiyozalisha lazima uone benk ni mchawi wako.
 
Mhh Kwa miaka 20 kiwango mbona kidogo sana.
Tuchukue update hizo milion 40 uwekeze mfano kwenye biashara ya utengenezaji wa unga wa sembe.
Kukodi jengo 300000*12'=3600000
Mashine ununuzi =8000000
Kuingiza umeme=2000000
Mifuko grade1 ya kuanzia(2000)=1000000
Mpaka hapo jumla=14600000
Unabaki na 25400000
Toa 25000000 kipind cha mavuno nunua Mahindra utapata kg 40000
TUJE KWENYE UZALISHAJI
Ukijiwekea target kila siku usage tani kumi Kwa wastan wa faida ya 300000 Kwa tani kumi. Hapa bila pumba.
Ukifanya Kwa siku 20 Kwa mwezi,
20*300000= utaingiza 6000000 Kwa mwezi.
Kwa mwaka 12*6000000=720000000
Kwa miaka 20*72000000=1.44bil
1.44bil-147mil=?

TUJE KWENYE DECISIONS
Kwa maono yangu tatizo sio benki Bali maono ya mtu na exposure.
Nipe Mimi hizo nikupe 200mil Kwa miaka miwili Ila au nipe machinery za that amount hiyo nichague eneo la kufanyiwa biashara nikupe mara kumi ya capital yako ndani ya mwaka.
Mkuu nimesoma post yako ingawa hujaandika details zote za gharama na changamoto zote lakini kupata hiyo faida inawezekana kama unauzoefu na mikakati bora ya biashara(better location,raw materials purchase ,efficient machinery and sound market strategy)

Nimeona baadhi wanavyokupinga natamani wajue wapo wachache wamefanikiwa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mikopo ya bank sio poa,
Ila naomba nikurekebishe hapo kwenye riba, hiyo riba ya 18% itakuwa calculated kwa deni litakalobaki kwa kila mwaka na sio kwa hell uliyokopa.
Mfano ukikopa 40m riba ya 1st year 7.2m
Then 2nd year deni Ni 32.6 riba 5.86m

So trend inaenda namna hiyo so sidhani Kama itafika 144m
hiyo unayoizungumza wewe ni reducing figure method, ikiwa inatumika
straight line method italeta matokeo tofauti

Hasara Umfika Mwenye Mabezo
 
Wasalamu wakuu.
Baada ya hawa jamaa wa benki kuja kutoa semina hapa lindoni kwetu wakanishawishi kweli kweli kupata mkopo wa Kujenga.
Sasa last week nikawaibukia ofisini kwao nikawaambia nataka 40,000,000 nirudishe kwa miaka 20 kama walivosema wao.
Leo nikapigiwa simu kuwa niende nikasaini tayari process zishafanyika. Nilipofika kusoma nikaona kama nimechoka naomba nichukue nikasome taratibu kisha nitarejesha.
Hesabu iko hivi.
Mkopo: 40,000,000.
Riba: 18% (annually)
Monthly payment: 617,325.00
Hapa ukipiga hesabu for 20 year nitalipa
617,325.00 * 12 * 20= 148,158,000/=
Yaani almost 4 times ya hela nilokopa.
Nimeamua kuchoma huu mkataba nimempigia afisa mikopo kuwa sitoweza kusaini aendelee na shughuli zake.
Hapa ndo naelewa wale wanaonunua tofali kila mwezi kuweka kwenye kiwanja.
Bank hamnipati tena.
Riba imekatazwa sana kwenye vitabu vya dini zote,

Chochote kile kilichokatazwa kwenye dini,
Ukikifanya hasara yake unaiona kabisa,

Sema tu ndio hivyo tunafanya ubishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi nilifatilia mkopo kwny taasisi furani ya mtu binafsi , sasa nilitaka kuchukua 10M sasa
Mchanganuo fomu 200,000
unatakiwa ukatie bima mkopo 1M
Unarudisha Mil 15
Ndani ya two years nikaona ushenz nikasepa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hauwezi kutoboa bila kukopa, wake zetu wajanja sana wao wana vyama vyao wapo wanaopeleka 2,000 kila wiki na wapo 10,000 kila mwezi.
wanakopeshana, sema mfumo wa riba yao na ukopeshaji haupo sawa sana.

niliwashauri mtaji ukishakua walau wapunguze kiwango cha riba maana riba yao ni 10% na mkopo ni mwezi mmoja.

na fomula ipo hivi, utake usitake ipo siku utakopa. sasa bora ukope kwa hiari kuliko kuja kukopa kwa msukumo wa changamoto, labda kuumwa, kuuguliwa, msiba.
tofauti na hapo basi ndio kuuza vitu vya ndani kwa bei ndogo.

kuliwa ni lazima ila ukiwa makini kidogo na mwenye nidhamu itakusaidia kupunguza maumivu.



Hasara Umfika Mwenye Mabezo
 
Wasalamu wakuu.
Baada ya hawa jamaa wa benki kuja kutoa semina hapa lindoni kwetu wakanishawishi kweli kweli kupata mkopo wa Kujenga.
Sasa last week nikawaibukia ofisini kwao nikawaambia nataka 40,000,000 nirudishe kwa miaka 20 kama walivosema wao.
Leo nikapigiwa simu kuwa niende nikasaini tayari process zishafanyika. Nilipofika kusoma nikaona kama nimechoka naomba nichukue nikasome taratibu kisha nitarejesha.
Hesabu iko hivi.
Mkopo: 40,000,000.
Riba: 18% (annually)
Monthly payment: 617,325.00
Hapa ukipiga hesabu for 20 year nitalipa
617,325.00 * 12 * 20= 148,158,000/=
Yaani almost 4 times ya hela nilokopa.
Nimeamua kuchoma huu mkataba nimempigia afisa mikopo kuwa sitoweza kusaini aendelee na shughuli zake.
Hapa ndo naelewa wale wanaonunua tofali kila mwezi kuweka kwenye kiwanja.
Bank hamnipati tena.

Unafuu wa mkopo kwenye mabenki ni pale tuu unapokuwa na uwezo wa kuurejesha kwa kipindi kifupi. Kardi muda wa marejesho unapokuwa mrefu vivyo hivyo utajikuta ukirejesha fedha nyingi kama ilivyo kenye case yako.
 
Sijakataaa kuwa kuna utitiri wa mambo kama tra na tfda Ila muhimu ni lengo rasmi na uchaguz wa eneo sahihi la biashara. Kinachokufanya wengi wetu ni kufanya biashara Kwa kuigana na kukosa lengo rasmi.
Kama umenisoma vizuri kwenye bandiko langu no kuwa kila ntakapo nunua mzigo wa 5mil nipate wastan wa faida ya 300k Sawa na 6%, katikati Hali halisi inazid Sana no karibia 800k Kwa sasa.
Kwa kila mzigo 5mil utatoa pumba walau 3000kg au pungufu. Kiroba kimoja cha kilo 100 kinaenda 16000tsh. Kwa mzigo wa 5mil utapata pumba ya dhaman 480000. Kumbuka hapo huu sikuweza pumba.
Kwa ujumla faida IPO Sana Tu. Ni mzoefu wa hii KAZI mitaji ya kuanzia ndo sumbufu jaman

Ok sio kuwa motivation speaker hapana Ila nikazi ambayo nimekuwa naifanya Kwa muda mrefu Sana.
Kwanza niwekee wazi nimezungumza hivo kulingana na mazingira niliyotukana nafanyaje Mimi.
Kingine ieleweke sio kila biashara lazima jifanye dar au Tanzania ambako Ile ki Hali halisi kupiga hiyo pesa itakuwa ngumu.
Tukija kwenye selection ya eneo ambako ndo Kwanza ntaweza pendekeza Kwa MTU yoyote mwenyewe mtaji WA kiwango hicho ni either aende Mozambique na hasa mkoa kama nampula au kigoma Kwa upande wa Tanzania.
Tukija kwanini kigoma na wala sio dar.
Kigoma kama kigoma(kigoma mjini) kuna uhaba Sana wa chakula inafikia hatua unga WA sembe unafika mpaka 40k na Kwa wasiojua tu, hapa dar es salaam ni ngumu kupata unga WA sembe wa Azam tokana na ushindan mkubwa lakini Azam anauza kigoma sana. Na pia tukumbuke kilichozuiwa ni kusafirisha Mahind sio unga.
Kuna challenge umezungumzia ushuru wa mazao. Kama unafungua kiwanda na ukategemea kuwa utakuwa unafuata Mahind mwenyewe shamban jua ndo anguko lako kama huna mtaji. Siri iliyoko ni wewe kusubiria wanunue wa vijijin wa

Nadhani niliposimamia na wewe ulipoelekea ni tofaut. Mimi sijazungumzia kufuata mahindi vijijini bali nimezungumzia kuwekeza katikati uzalishaji. Katika uzalishaji wowote lazima utegemee kuwa na suppliers wa mzigo au Kwa lugha nyingine Mali ghafi. Kwa hapa bongo ni madalali. Na hawa kuna wengine wanaweza kukuletea mzigo mpaka Kwa mkopo na wewe ukapigana kuuuza bidhaa zako uliyotengeneza.
Kwa hiyo wewe utadili na tfda,tra, tanesco, na vipimo.
Tukija kwenye gharama za uendeshaji.
Karibia kila gharama itaendana na uzalishaji wako.
Mara nyingi huwa hatuajiri Kwa mishahara Bali tunategemea vibarua kuanzia kukoboa,kusaga na hata kuuanika na kuuza pumba( ndo maana ukienda nunua pumba au ukienda mbagala kununua mchele au unga unakutana na gharama ya ubebaji au kupimiwa.
Challenge kubwa ni ni soko ambalo wengi wetu tunafanya kimazoea ni wachache Sana ambao wamebadilika na wanaenda kisasa kuendana na soko lakini Siri kubwa chakula hatuaez Acha Kula. Tena mahindi yanapopotea kwetu n neema.
Gharama ambazo kwangu naona ndo ngumu ni zile za mwanzo kama ununuzi wa mashine, usajiri was kampuni, ujenzi uingizaji wa umeme.
Tukija upande wa pili kinachowashinda wengi ni pale mwanzon unataka uwaachie watu wakufanyie weww uletewe mauzo hutayapata sio dalala hiyo.

Naongelea kitu ambacho nalijua kama unapesa njoo nikupe location usajiri kila kitu Kwa jina lako nipe mwaka mmoja nikupe hela yako

Hapo uliposema usinunue mwenyewe kutoka shambani sijaelewa nilidhani ukinunua mwenyewe ndio itakuwa nafuu
Ni kweli biashara ya chakula haiwezi kufeli watu wanahitaji kula kabla ya chochote kingine
Tatizo ni soko na location kama ulivyosema inamaana kwa Tanzania ni kigoma tu ndio sehemu sahihi?
 
Back
Top Bottom