Leo nlipita ktk bank 5 tofauti kuulizia taarifa za mikopo kwa wajasiliamali:niliwatembelea CRDB,NMB,TPB.Barclays na MUCOBA, kifuatacho ndicho nilichokipata:
1. CRDB,NMB,TPB na MUCOBA
Hawa jamaa wanakopesha wafanyakazi wa serikali au mfanyabiashara mwenye biashara tayari inamaana kwa sisi tunaohitaji mtaji kwaajili ya kuanza biashara hatuna nafasi regardless una asset gani ya dhamana..
Mfano mimi nina kiwanja kimepimwa pia kinajengwa lakini wamesema sina nafasi kwakuwa sina biashara inayorun.
2. Barclays wao ndo hawana mpango kabisa wa kukopesha mjasiliamali.
Kiukwel nimehuzunika sana kwa ubaguzi huu nina asset to be used as security bado nafanya kilimo lakin sikopesheki?, dah tufanyaje sisi??