Banza Stone ana hali mbaya

Half London

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2014
Posts
261
Reaction score
112
Aliyekuwa mwanamuziki wa Twanga Pepeta,Ramadhani Masanja au Banza stone,anaumwa sana na yuko Mbeya. Habari zinasema kakosa hadi nauli ya kurudi Dar Es salaam. Mkurugenzi wa Twanga pepeta Asha Baraka,kasema yeye atamtumia tiketi kwani hawezi kumtumia pesa. Yuko maeneo ya Tunduma pamoja na msanii mwenzake wa zamani wa Twanga anayeitwa Athanas. Source: Radio Tumaini na Luiza Mbutu.
 

unga mbaya sana daah.
 
Banza amekula ujana sana..saivi ujana unamla yeye..unga ni hatari sana usifanye mchezo..leo hii Banza ni wakukosa nauli ya kurudi Dar kweli!!?
 
Asha atakua na tatizo kwenye kumanage wasanii wake...kwanini wanaathirikia kupita kiasi na unga na bangi wakiwa chini yake. Madinda, chokoraa; diof, banza nk. Anasubiri wafe agharamie mazishi? Hawa wasanii wamemtajirisha sana anatakiwa awafanyie zaidi ya kuwatumia tiketi!
 

Nawao wasanii wanatakiwa kujitambua!
 

Wao ni watoto wadogo mpaka awachunge. Yeye hameneji tabia za mtu binafasi, anameneji bendi!
 
Kama orodha hiyo ndefu ya watumiaji labda anawalipa uzuri! au anawalipa kiduchu wanakuwa na stress?
 

hawezi wazuia kubwia na kuvuta kwan ni personal interest
that's y inakuwa hivi
mara nyingi boss anaangalia kama kaz yake inaendamengine is upto yeye mwenyewe
 
Unga (madawa ya kulevya) ni donda ndugu Tanzania.
Vijana tusifanye mistake October 2015.
 
Diouf alienda kumshtaki Banza kwa Asha Baraka kwamba anawafundisha Aisha na wenzake wawili wa kike,nao ni wacheza show. Banza hiyo kitu akakataa,Diof alikuwa hataki hao mademu wavute nao. Ingawa na yeye alikuwa anatumia. Diouf sasa hivi yuko England,kamfata mama watoto wake.
 
Sanaa ya bongo nzito,ukitaka kuwa maskini maarufu basi fanya sanaa Tz,huyu jamaa tangu atangaze kuwa siku zake za kuishi si nyingi sikumsikia tena ila Dunia ni mapito ipo siku...
 
Huwezi katu kumlaumu mwajiri wa mtu kwa sababu ya utumiaji wa madawa ya kulevya. Asingeweza kjmlinda, kama ambavyo hata mzazi hawezi kumlinda kijana wake asitumie madawa. Siku banza agakapogundua kuwa uamuzi wa kufa ama kuishi uko mikononi mwake ataanza kuwajibika na kujiokoa
 
Banza amekula ujana sana..saivi ujana unamla yeye..unga ni hatari sana usifanye mchezo..leo hii Banza ni wakukosa nauli ya kurudi Dar kweli!!?

Wabongo walivyo wanafiki sasa, japo hatuombei itokee, akifariki ndio utasikia redioni nyimbo zake zitapigwa na kurudiwarudiwa kutwa na wauzaji wa cd watauza sana, na msibani wasanii watajiliza sana na kujifanya wamezimia, utaona miguo imevaliwa mieusii na mamiwani meusi makubwa, kila msanii atakayehojiwa na tv atakuwa na kitambaa cha kufuta machozi na kujifanya wana uchungu mno! Hebu msaidieni Banza leo sio mngijee afe mtafute sifa.
 
Pole sana Banza Stone. ninachofahamu ni kuwa leo atalala Mbalizi then asubuhi atawahishwa kwenye Ndege uwanja wa Songwe arudi Dar. Masuala ya tiketi ya bus imetupiliwa mbali na rafiki yake kipenzi alieshiriki BSS 2008/2009. Rahim Nzunda
 
Reactions: G3T
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…