Bar/pub na mziki mkubwa: Wenye bar tambua kuajiri mameneja na ma dj maskini wa kufikiri inawaharibia biashara

Bar/pub na mziki mkubwa: Wenye bar tambua kuajiri mameneja na ma dj maskini wa kufikiri inawaharibia biashara

Lububi

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2013
Posts
2,158
Reaction score
3,808
Heshma kwa wadau rika zote.

Nadhan tumeshakubaliana kuwa hasa tuishio mjini imeshakuwa tabia mbaya kurudi nyumban mapema sana baada ya mihangaiko.

Isitoshe mipango hufanyika bar sio kufuatana majumban!
Na hivi wenye wake wanakwepa visiran vya wenza ili zisitolewe saba mkupuo.

Unakuta mke hajakamilisha idad ya maneno yake kwa siku, utaulizwa hata kitu cha kukuharbia siku tu.
Basi tu vile ndoa ni dying institution kila kiumbe kitaishi kwa kujinafasi kivyake. Na onenight stands za hapa na pale.

Sasa nije kwa wamiliki na mameneja wa bar na pubs washamba wa muziki. Dj anaokotwa huko kijiwe cha kuuza cd anayapiga maspika akidhan anafurahisha wateja kumbe ndo anawafukuza mazma. Hakuna cha kujadili kwa mziki ule.

Wenye bar mmewekeza ili mpate hela sasa wadhibiti wasimamiz washamba wa starehe hawa. Hizo kelele zinafukuza wateja hasa wastaarab. Mnabaki na wanywaji wa double kick.

Mziki uwe kiwango cha kuruhusu watu kuongea. Ikibid ma dj wenu muwe mnawapima na akili.
 
uache kwenda vilabuni sasa....wenzako wanaenda club wewe unaenda kilabuni.. afu unataka balanced sound..
 
uache kwenda vilabuni sasa....wenzako wanaenda club wewe unaenda kilabuni.. afu unataka balanced sound..
Kaka hauishi mjini nini. Kama uko goziba au murusagamba huwez kunielewa. Ni hivi, kila bar kubwa na ndogo kuna dj. Sasa tatizo ni ukubwa wa sauti sio wa kumfanya mteja ajihisi kukaa sehem hiyo tena! Na unakuta huduma nyingine nzuri tu. Sitaki kutaja kulinda biashara za watu lakin wilaya ya ubungo hasa bar za kimara imezidi.
 
kweli aisee unakuta mtu umeenda kupata tulite twako tuwili ili uvute muda uende home unakutana na noise pollution ya hatarii
 
Miongoni mwa watu wanaokwazika na huo mziki ni mimi,hakuta utulivu,ukipigiwa simu unatimua bio kwenda nje ukapokee vizuri,ya nini yote hayo
Aisee kweli tuko tofauti, mimi huwa napenda Bar zenye mziki mnene au live band, nikikuta bar imetuliaa nahama...
 
Nami sipendi sauti kubwa unakuta mnapiga story kwa shida sana,,,mnaongea kama mpo kwenye mashine ya kusaga bana
 
Back
Top Bottom