Bar za Babati na Limbwata la pombe: Njoo ushuhudie!

Bar za Babati na Limbwata la pombe: Njoo ushuhudie!

ndyoko

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,971
Reaction score
1,652
Wamiliki wa baadhi ya baa za mji wa babati wamekuja na mtindo mpya. Huu unahusisha kuwawekea dawa za kienyeji wateja wanaowaona wana hela ili wawe wanywaji wa kudumu kwenye baa zao hali inayowafanya waingize kipato kizuri kupitia wanywaji hao.

Hutokeaje? Wamiliki wakishajua wewe ni mtu mwenye nazo, wanangoja uende chooni, wao kwa kuwatumia watu unaokunywa nao, wanaweka hilo 'limbwata' kwenye pombe iliyomo kwenye chupa au glasi. wewe ukirudi na kufakamia hicho kinywaji, ndo ntolee.

Hii imeshawatokea watu sita ninaowajua ambao hadi sasa wamefilisika kabisa kwani waligeuka na kuwa wanywaji wa pombe toka asubuhi hadi usiku wa manane. Hata kwenda kazini kwao ilikuwa ni vigumu. Wakiamka ni kwenda baa, baada ya kazi ni baa.

Kwa wageni mnao au mtakaotembelea babati, habari ndo hiyo...........wambulu wameamua kuja kivingine kabisa, kazi kwenu!
 
Si baa tu hadi madukani

C.C Preta
 
Last edited by a moderator:
asee kwa hiyo hata kama umepita kwa usiku mmoja unakamatwa?
 
we mwongo.. siamini hayo mambo ya limbwata, kama watu hao wamefilisika kwa ajili ya unywaji wa pombe basi utakuwa uzembe wao. otherwise tupe confirmation.
 
we mwongo.. siamini hayo mambo ya limbwata, kama watu hao wamefilisika kwa ajili ya unywaji wa pombe basi utakuwa uzembe wao. otherwise tupe confirmation.

Mbulu ipo unapigwa kitu kinaitwa "kifafi"
 
mkuu mleta mada kwa upande moja nahisi unawasingizia hoa wwamilik kwasababu zifuatazo

1. we umetaja wambulu wote ( generalization) je? hakuna makabila mengine zinazofanya au kumiliki biashara za bar kwa hapo babati?
2.idadi ya sampuli (sample used) ya watu sita ni ndogo sana ukilinganisha na idadi ya wakazi wote wa babati
3. una ushahidi gani kuwa hao wamiliki ndo wanafanya hvyo?
kwa uelewa wangu suala la mtu kuwa mlevi wa kupitiliza husababishwa na mambo mengi kama vile stress za maisha, pili jamii inayomzunguka ikiwemo jamaa na marafiki wenye wivu mbaya wa maendeleo tuseme roho mbaya kwani humfanyia mwenzao hvyo ili asipate na asiwaze maendeleo
ni hayo tu mwenye ziada ruksa kuendeleza
 
mkuu mleta mada kwa upande moja nahisi unawasingizia hao wamiliki kwasababu zifuatazo

Back
Top Bottom