Bar za Tabata zinajaa sana, Magufuli endelea kukaza

Bar za Tabata zinajaa sana, Magufuli endelea kukaza

hii sasa shida.. unamshauri mkuu ashughulikie bar!!!!!!
 
Kwani "hapa kazi tu" haina matunda? Hao wanakula 'matunda' ya "hapa kazi tu'. Kwa upande mwingine huoni kama wanaiongezea serikali mapato? Kazi wanazofanya unazijua? Pia huoni kama wanatunza ajira ya viwanda vya bia kama wanatumia bia zinazozalishwa hapa nchini?
 
No kupangiana kila mtu anafanya nnachojisikia Mkuu

Acha wanywe zao tu angalia yako
 
Tabata kuna bar mpya zimefunguliwa mfano The great Park, 40 by 40, kwetu pazuri, kwa kweli zinajaza sana watu.

Ukitembelea hizi bar alafu ukasikia mtu analalamika hela imepotea mfukoni hautamwamini kamwe.

Watu wanapiga mitungi kama kawa mpaka majogoo.
kuna nyingine ipo tabata kinyerezi pale inaitwa new makirikiri isee ni balaa,gari zimejaa msururu na hakuna gari ya kichovu, basi watu walivyo na mbwembwe unaona anajidai amesahau powerbank anampa barmaid mzuuuur funguo za gari anamtuma hebu nenda kwenye gari pale T654 DDD Prado new model chek siti ya nyuma kuna powerbank uniletee,HAPO UJUE AKICHOMOKA ANACHOMOKA NA HUYO MTOTO.
 
Mme mjibu vizuri.. . .
Naamini hata waliokua na mawazo ya kupost hoja za namna hii watajitafakari mara mbili.

Nadhani ni mtu Kama wewe unatamani watu wote watembee kwa miguu,

Wale mlo mmoja.
Sa sijui wengine wasipo jifurahisha wewe unafaidika nini?
Roho mbaya tu na wivu wa kipuuzi
 
Uchumi wa marekani uko juu kwasababu ya consumerism,

kadri unavyofakamia kwa kasi ndo pia unachangamsha uzalishaji zaidi na hivyo ajira zaidi,

kama watu wanajaa sana pale,ina maana bia zitanyweka sana ,mishikaki italika sana,kuku watatafunwa sana etc,
hapo umeongeza ajira kwa muuza mkaa,muuza nyanya,karoti,kitunguu,chumvi na kabichi,
mafuta ya kula,
umeongeza ajira kwa wakulima wa vitu hivyo na wabeba mizigo wanaoushusha bia,viwanda vya bia vinaongeza uzalishaji,watu wanapata ajira na kupeleka watoto shule,mwenye shule nae amepata kipato tokana na kodi hiyo,
changudoa nae kapata ajira na pesa analipa pango ,analipa ada za watoto na anatuma hela za kulimia kijijini etc.

Kama sizonje hajui hili mumueleweshe
consumerism= spendthrift?
 
Mme mjibu vizuri.. . .
Naamini hata waliokua na mawazo ya kupost hoja za namna hii watajitafakari mara mbili.

Nadhani ni mtu Kama wewe unatamani watu wote watembee kwa miguu,

Wale mlo mmoja.
Sa sijui wengine wasipo jifurahisha wewe unafaidika nini?
Roho mbaya tu na wivu wa kipuuzi
Mtanyooka tu
 
kwetu pazuri
haya mambo jamaa hataki kabisaaaa kuyasikia atawaita nyie ni wapiga dili
 
Tabata kuna bar mpya zimefunguliwa mfano The great Park, 40 by 40, kwetu pazuri, kwa kweli zinajaza sana watu.

Ukitembelea hizi bar alafu ukasikia mtu analalamika hela imepotea mfukoni hautamwamini kamwe.

Watu wanapiga mitungi kama kawa mpaka majogoo.
Nashindwa kuelewa nikuweke kwenye kundi la wenye wivu ama fungu la kukosa? Sasa akibana zaidi hizi bar zikafungwa hao TBL pesa za kulipa kodi na mishahara ya watendaji wao zitatoka wapi?
 
Huu ni mwisho wa mwezi lazima zijae nenda katikati ya mwezi
 
Back
Top Bottom