_BY MZEE WA ATIKALI_ [emoji871][emoji871][emoji871]
_*"Everytime you see Hon. Dr. Hussein Mwinyi in public, you immediately note that he has a Statesman's demeanor, looks and sounds Presidential"*_.
THOMAS J. KIBWANA, 19.6.2020
1. *Usuli*
Ibara ya 18(1) ya Katiba ya Tanzania 1977, kama ilivyorekebishwa, inaeleza-:
_*"........Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, kupokea na kutoa habari kupitia chombo chochote..."*_.
_MZEE WA ATIKALI_ anatembelea kwenye Ibara hii kutoa maoni yake kuhusu suala la Urais ambalo ni muhimu sana kwa mustakabali wa Taifa letu.
_ATIKALI_ ya leo inamuhusu Mh. Dr. HUSSEIN ALI HASSAN MWINYI ambaye _MZEE WA ATIKALI_ anamuona ana sifa zote za kuwa Rais wa awamu ya nane wa Zanzibar, na panapo majaliwa kuja kuwa Rais awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano mwaka 2025.
Je, Dr. HUSSEIN alizaliwa wapi, lini, alisoma wapi, uzoefu wake ni upi na kwanini ana nafasi kubwa ya kuwa Rais?
*Twende pamoja.......*
2. *Kuzaliwa*
HUSSEIN alizaliwa Zanzibar siku ya Ijumaa, tarehe 23.12.1966, akiwa ni mmoja wa watoto 12 wa Mh. ALI HASSAN MWINYI, Rais wa awamu ya pili TZ.
3. *Elimu:*
3.1 *Elimu ya Msingi & Sekondari*
HUSSEIN alipata elimu ya msingi _"Oysterbay Primary School"_ kuanzia mwaka 1974. Enzi hizo hii ndio ilikuwa shule bora ya msingi TZ.
Mh. Mzee MWINYI alipojiuzulu uwaziri wa Mambo ya Ndani mwaka 1976 na kuteuliwa kuwa Balozi nchini Misri alihama na familia yake.
Hivyo, HUSSEIN alisoma Misri katika shule ya _"Manor House Junior School"_ kuanzia 1977.
Mzee MWINYI aliporejea nchini, HUSSEIN akajiunga na _"Azania Secondary School"_ kisha _"Tambaza Secondary School"_.
3.2 *Chuo Kikuu*
HUSSEIN alipata Shahada ya Utabibu _"Doctor of Medicine"_ huko _"Marmara University, Instanbul, Turkey"_ na baada ya hapo akapata _"Masters"_ na PhD huko _"Hammersmith Hospital"_ UK.
4. *Ajira*
4.1 *Muhimbili*
Mwaka 1993, HUSSEIN akawa daktari Muhimbili na mwaka 1994 akawa Msajiri.
4.2 *Hubert Kairuki*
Mwaka 1998-99, Dr. HUSSEIN alikuwa _"Specialist doctor"_ pale _"Hubert Kairuki Memorial University"_, Mikocheni, Dsm.
Mwaka 1999, Dr. HUSSEIN akawa _"Lecturer"_ chuoni hapo.
5. *Ubunge*
Mwaka 2000, Dr. HUSSEIN aligombea ubunge jimbo la Mkuranga, Pwani na kushinda kwa kishindo.
6. *Rais MKAPA Amteua Mh. Dr. HUSSEIN Kuwa Waziri*
Mwezi Desemba 2000, Rais MKAPA alimteua Mh. Dr. HUSSEIN kuwa Naibu Waziri wa Afya.
7. *Rais KIKWETE Amteua Mh. Dr. HUSSEIN Kuwa Waziri*
Tarehe 6.1.2006, Rais J. KIKWETE alimteua Dr. HUSSEIN kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya VP, Muungano.
8. *Rais KIKWETE Amhamisha Wizara Mh. Dr. HUSSEIN*
Tarehe 13.2.2008, Rais KIKWETE alimteua Dr. HUSSEIN kuwa Waziri wa Ulinzi & Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
9. *Rais KIKWETE Amuhamisha Tena Wizara Mh Dr. HUSSEIN*
Tarehe 7.5.2012, Rais KIKWETE alimteua Dr. HUSSEIN kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.
10. *Rais KIKWETE Amrudisha Mh. Dr. HUSSEIN Wizara ya Ulinzi*
Tarehe 14.1.2014, Rais KIKWETE alimteua Mh. Dr. HUSSEIN kuwa Waziri wa Ulinzi na JKT.
11. *Dr. JPM Amteua Mh. Dr. HUSSEIN Waziri wa Ulinzi*
Mwezi Desemba 2015, Rais wa awamu ya tano, Mh. Dr. MAGUFULI alimteua Dr. HUSSEIN kuwa Waziri wa Ulinzi & JKT.
12. *KINYANG'ANYIRO CHA URAIS ZANZIBAR*
12.1 *Mh Dr. SHEIN Anan'gatuka*
Mh. Dr. ALI MOHAMED SHEIN anamalizia muhula wake wa pili kama Rais wa 7 wa ZNZ. Hivyo, mchakato wa kumpata Rais wa 8 wa Zanzibar ndio umeanza.
12.2 *Makada wa CCM Watia Nia*
Mwezi Juni 2020, Makada 32 wa CCM walichukua na kurudisha fomu za kugombea Urais ZNZ ili kumrithi Dr. SHEIN.
12.3 *Dr. HUSSEIN Amuiga Dr. JPM*
Dr. HUSSEIN alienda kuchukua fomu Afisi ya CCM Kisiwandui, siku ya Jumatano, tarehe 17.6.2020 saa tisa alasiri. Dr. HUSSEIN alikuwa kada wa tano wa CCM kuchukua fomu.
Kama ilivyokuwa kwa Dr. JPM mwezi Julai 2015 Idodomia, Dr. HUSSEIN nae alikataa katakata kuongea na waandishi wa habari, tofauti na wagombea wenzake ambao walidadavua kwa kirefu sera zao. Dr. HUSSEIN, kwa unyenyekevu mkubwa, alitiririka-:
_*"Nawaombeni radhi ndugu zangu waandishi kwani mimi leo sikuja kuongea na waandishi wa habari kwakuwa jukumu langu lilikuwa ni kuchukua Fomu tu. Hata yaliyomo kwenye Fomu siyajui hivyo niruhusuni nikaisome, niijaze kisha nitekeleze mambo yanayotakiwa na kuirudisha Fomu hii kabla ya muda. Asanteni sana"*_.
12.4 *KAMATI MAALUM _"Yawachinjilia Baharini"_ Wagombea 26*
Kwa mujibu wa Mh. ABDULLA MABODI, Naibu Katibu Mkuu, CCM, ZNZ, jumla ya Wagombea 32 walichukua fomu na mmoja hakurudisha.Jumamosi ya tarehe 4.7.2020, Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu (Taifa) Zanzibar ilipitisha majina 5 na kukata majina 26 baada ya kupitia fomu na taarifa ya kila mgombea.
12.5 *CC _Kufyeka_ Majina 2*
CC ya CCM itakayoketi Idodomia siku ya alhamis, tarehe 9.7.2020, itayapitia majina hayo 5 na kuona kama yanakidhi vigezo 12 vilivyowekwa kisha itayapeleka majina 3 kati ya hayo Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).
12.6 *NEC Kupendekeza Jina la Mgombea wa CCM*
Siku ya Ijumaa, tarehe 10.7.2020, NEC itayapokea majina hayo 3 kisha kuchuja 2 na kulipeleka kwenye Mkutano Mkuu jina 1.
12.7 *Mkutano Mkuu Kuthibitisha Jina la Mgombea*
Jumamosi ya tarehe 11.7.2020, Mkutano Mkuu utathibitisha jina la mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM lililopendekezwa na NEC.
13. *"Dr. HUSSEIN MWINYI Anatosha ZNZ*
Kwa kuzingatia vigezo ambavyo huwa vinatajwa miaka yote ya uchaguzi nchini, _MZEE WA ATIKALI_ amewiwa kutoa maoni kuwa Dr. HUSSEIN anakidhi vigezo vyote, hivyo anatosha kuibeba bendera ya CCM na hatimaye kuwa Rais wa ZNZ ifikapo mwezi Novemba 2020.
14. *Dr. HUSSEIN Kuwa Rais Wa TZ 2025?*
_MZEE WA ATIKALI_ amewiwa pia kutoa maoni kuwa Dr. HUSSEIN ana nafasi kubwa ya kuja kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TZ mwaka 2025, kwasababu Mujarab zifuatazo:
14.1 *Rais Mpya wa Awamu ya 6 TZ Atapatikana 2025*
Mh. Rais Dr. MAGUFULI atakuwa anamaliza muhula wake wa pili na wa mwisho Kikatiba, kama _Bongolanders_ wengi tuaminivyo kuwa atashinda kwa kishindo 2020, hivyo 2025 itakuwa ni fursa kwa mgombea mpya;
14.2 *Hoja ya MUUNGANO "itambeba"*
14.2.1 Dr. HUSSEIN ni muumini mkubwa wa Muungano. Muungano ni kitu muhimu sana hivyo ni lazma tujiridhishe pasina shaka kuwa tunaemchagua kuwa Rais ataulinda Muungano wetu huu wa kipekee duniani;
14.2.2 *Dr. HUSSEIN anauakisi Muungano*
Dr. HUSSEIN ndiye Mtanzania pekee aliyewahi kuwa Mbunge wa pande zote za Muungano. Alianza kuwa mbunge Bara (Mkuranga 2000-2005) na kisha Visiwani (2005--, Kwahani);
14.2.3 *Dr. HUSSEIN Amewahi Kuwa Waziri wa Muungano*
Dr. HUSSEIN amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Rais, hivyo matatizo na changamoto za Muungano anazielewa vizuri;
14.3.4 *Dr. HUSSEIN anapendwa sana Wizara ya Ulinzi*
Dr. HUSSEIN anapendwa sana Wizara ya Ulinzi, ambayo ni ya Muungano, kutokana na utendaji kazi wake kuntu na kujali na kufuatilia stahili za Wanajeshi.
14.2.5 *Itapendeza 2025 Rais akitoka ZNZ*
Toka Tanganyika iungane na Zanzibar tarehe 26.4.1964, zimepita awamu tano za Urais wa Muungano ambapo Mzanzibar amekuwa Rais kwenye awamu moja tu hivyo itapendeza Rais wa awamu ya sita atoke ZNZ.
14.3 *Dr. HUSSEIN Ana Uzoefu Mkubwa*
Dr. HUSSEIN amekuwa mbunge na Waziri kwa miaka 20 hivyo ana uzoefu wa kutosha wa uongozi;
14.4 *Dr. HUSSEIN ana Haiba ya Uongozi*
Dr. HUSSEIN ni mtu mwenye haiba ya uongozi, mnyenyekevu, mkarimu na mcha Mungu.
14.5 *Dr. HUSSEIN Hana Kashfa*
Dr. HUSSEIN ni mtu aliyelelewa kwa maadili na asiye na tamaa za mali na ndio maana hana kashfa yoyote.
14.6 *Dr. HUSSEIN Alisifiwa na Rais Dr. JPM*
Tarehe 27.1.2020, Mh. Rais Dr. JPM alipokuwa akimuapisha Mh. GEORGE SIMBACHAWENE kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alimsifia sana Dr. HUSSEIN kwa utendaji wake wa kazi Mujarab na kumtaka Mh. SIMBACHAWENE aige utendaji huo wa Dr. HUSSEIN.
14.6 *Dr. HUSSEIN Atafuata Nyayo za _"MZEE RUKSA"_*
Rais MWINYI@ _MZEE RUKSA_ alikuwa Rais wa ZNZ toka tarehe 30.1.1984 hadi tarehe 24.10.1985 na akawa Rais wa TZ toka tarehe 4.11.1985 hadi tarehe 4.11.1995.
Hivyo, Dr. MWINYI nae atakuwa Rais wa ZNZ, iwapo atapitishwa, kisha atakuwa Rais wa Muungano.
15. *TAMATI:*
Haya ni MAONI tu ya _MZEE WA ATIKALI_ kama aonavyo yeye kwani ni haki ya kikatiba ya kila mmoja kutoa maoni yake ili mradi asivunje sheria za nchi.
Maoni haya yamezingatia jinsi _MZEE WA ATIKALI_ anavyomfahamu Dr. HUSSEIN, vigezo vinavyotumikaga wakati wa uteuzi wa Urais, sifa za Dr. HUSSEIN na Mustakabali wa Taifa letu.
KILA LA KHERI _CAMARADA_ Dr. HUSSEIN ALI HASSAN MWINYI!!!
_BY MZEE WA ATIKALI_ [emoji871][emoji871][emoji871]