Zanzibar 2020 Bara hatuwezi mweka Rais Zanzibar ambaye hatumfahamu vizuri. Tutamweka Mwinyi

Yooote haya hayamuombei. Rais wa Zanzibar anachaguliwa Dodoma na wala haijalishi CV ya mtu au matakwa ya Wazanzibari bali uongozi wa juu wa Chama. Safari hii wenye chama wanamtaka Prof Makame Mbarawa. Period
 
Kwamba Hussein Mwinyi anadharau!!!!!!? Hussein Mwinyo yupi unamzungumzia? Hapana ndugu yangu kwa hilo nakukatalia. Mtafutie dosari nyingine

Hussein Ali Hassan Mwinyi ni mpole, muungwana na mnyenyekevu sana kama kweli unayemzungumzia ni Hussein Mwinyi huyu ambaye anaomba ridhaa ya CCM kugombea urais wa Zanzibar. Ukweli ni kwamba kwa bahati mbaya wenye chama hawatampa fursa za kupeperusha bendera ya chama chake. Mizengwe kazini
 
Uchaguzi kwa watu toka Zanzibar haujawahi kuwa baridi kwenye kamati za ccm.
Wazanzibari wana mtandao waliwahi kumtisha mpaka baba wa Taifa
Nyerere.
Nyerere alimpenda na kumuamini sana Salim Ahmed Salim,
Watu walifunga safari mpaka dodoma na kumwambia mzee huyo ni hizbu,hajawahi kuwa na kadi ya ASP,Ukimpitisha kadi zako hizo hapo baba wa Taifa na umahiri wake alilegea
 
Mkuu, Wazanzibari walimtisha Mwl. Nyerere kwenye suala la Komandoo Salmin Amour. Kumbuka kwenye Urais wa Jamhuri ya Muungano Dr Salim Ahmed Salim hakuwa na nia wala hakuchukua fomu mwaka 1995

Wazanzibari wakati huo walipata tetesi kua kuna njama za kukata jina la Dr Salmin Amour Juma ambaye alikua Rais anayeomba tena uteuzi wa kipindi kingine na walienda Dodoma wakiwa na msimamo wa ama kurudi na jina la Salmin kama mgombea wao au warudi na Afro Shiraz Party kwa maana wanaachana na CCM

Mwalimu alirudi nyuma japo hakua amependezwa na uongozi wa awali wa Dr Salmin, na kama utakumbuka vizuri Mwl. alimsema sana Salmin baada ya kuponea chupuchupu kwenye matokeo ambayo CUF walidai Seif Sharif Hamad ameshinda, na hata televisheni ya DTV wakati huo ilimpa pongezi Maalim Seif na ikawa chanzo cha kutungwa sheria kwamba hakuna ruhusa chombo chochote kutangaza matokeo ya Urais wa Muungano au wa Zanzibar kabda ya tume za Uchaguzi za NEC na ZEC
 


MBALAWA
 
mkuu Zenji should remain a colony for a millenium!! hatujitoshelezi kiusalama! faida za kuisimamia Zenji ni nyingi kuliko hasara!!

Faida kwa wazanzibari kubakia kuwa koloni la Tanganyika (binafsi ni mzanzibari). Kama muislamu kutokea Zanzibar, Tanganyika ni nafasi muhimu ya kulingania dini ya kiislamu mikoani ukizingatia Zanzibar wasio waislamu ni wachache.

Nawashauri wazanzibari wenzangu wakajikita na hili hadi nusu karne ijayo tuwe tumamliza kazi inshallah.

Tuendelee hadi millenium!
 
Zanzibar hawatamweka bali watamchagua mgombea ambaye wanaona atawaletea maendeleo ila wewe una uhuru wako wakuchagua lakini usituchagulie bali wingi wa kura ndiyo utaamua.
 
Kwa CCM kuzaliwa bara sio issue..Jiwe kazaliwa nchi ya ng'ambo na kawa raisi....
 
Mkuu usisumbuke sanaaa rais wa zenji bara ndio tunampendekeza na nyie kaz yenu ni kumpigia kura tu hata msipomtaka atakalia kiti kwan 2015 si mlitaka maalim seif???? Vp alikalia kiti??? Ili uwe rais zenji lazima ukubalike bara tena bila chembe ya mashaka kuwa utalinda maslahi ya muungano. Hapa unamsema Mwinyi au hujui hata babaake Hussein nae kawa rais zanzibar lakin kazaliwa mkuranga bara????
 
Umenena vizur na kweli tupu lakin umesahau jambo moja muhimu sanaaa zanzibar ina historia ya tofaut za kisiasa zilizojaa chuki baina yao ASP na HIZBU hapa ndo shida ilipo na ndo ngao ya watanganyika kuwatawala na watatawaliwa milele mpaka watakapoelewana wao na kujiona ni wamoja baaaaasiiii hapo hata muungano utavunjwa wachache wanaelewa hili na karume jr kwa kuelewa hili akaanza na SUK kwanza hapa alicheza kama pele heko kwake ima wahafidhina nao wakamstukia hivuo wakafanya yao ili SUK ife then warud kulekule kwenye mapimduz daimaaaa ndan ya muungano madhubuti...binafsi I feel sorry for zanzibar kifupi wameuza nchi yao kwa tamaa ya madaraka ya watu wachache na wako kwenye mtego ambao hawawez kutoka. Wanaweza kutoka kama wakiacha tofaut zao za kisiasa jambo ambalo ni gumu pia kwao....MAPINDUZIIIIIIIIII
 
Duh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waafrika tuna matatizo makubwa sana.

Wenzetu huko kwa wazungu taifa moja linakuwa ni muungano wa mengine 52 na huwezi sikia lolote , ila hapa nchi mbili tu kila siku maneno.

Punguzeni tamaa jamani.
 

Yaani siamini tuko katika mwaka 2020 na bado kuna watu nchini Tanzania wanadanganyika na maneno ya tangu enzi za uhuru, eti wakoloni na waarabu wanaitaka nchi! Hivi hadi leo watu hamjaelimika juu ya kile kinachoitwa international relationship na pamoja na uwepo kwa umoja wa mataifa?

Hivi wewe kweli unaamini mwarabu anaitaka zanzibar kwa sababu gani? kuna nini zanzibar ambacho kitamfanya mwarabu achukue risk ya kutengwa na kushambiluwa na mataifa yote duniani kwa sababu tu ya kuivamia zanzibar? Sijui una umri gani lakini ni lini au mwaka gani uliwahi kusikia kuwa waarabu walijaribu kuivamia zanzibar, ni mwaka gani ulisikia kuwa kikundi fulani kimekamatwa nchi tanzania kwa kutuhumiwa kula njma za kumresha mkoloni nchini.

Siamini kabisa yaani tuko mwaka 2020 na bado kuna watanzania wenzetu wanachezewa akili zao na wanaendelea kutishwa na viongozi kwa maneno ya kuwa kuna wakiloni au masultani wanataka kuichukua zanzibar au tanzania kwa ujumla.

Hivi vitisho walikuwa wakitumia viongozi wa awali baada ya uhuru wa nchi zetu, ilikuwa ni njia rahisi sana ya kuweza kuwamiliki wananchi na kupata usalama nchini. Kwa vile wakati ule kila mwananchi alikuwa na kumbukumbu mbichi sana ya utawala wa wakoloni na masultani, hakuna ambae alikuwa anataka kurudi katika hali ile, na viongozi walijua hilo na kwa hiyo ilikuwa rahisi endapo mtu yeyote yule akitokea kuchallege serikali kusingiziwa kuwa ametumwa na wakoloni au sultani na ilikuwa rahisi kwa wananchi kuamini. Hii ndio sababu hapakuwepo vyama vya upinzani na wachache tu walithubutu kuuliza uongozi wa Nyerere.

Lakini leo mwaka 2020, kuona kuwa kuna watu wanaamini hili inasikitisha mno. Hebu fikiri ni nchi gani duniani ambayo iko tayari kuhatarisha maisha ya wananchi wake, kutengwa na mataifa yote duniani na kuondolewa katika umoja wa mataifa kwa sababu tu ya kuivamia Tanzania? Jiulize kuna nini Tanzania ambacho nchi nyengine iwe inataka kujitwika umiliki wake? Ni nchi gani au mtu gani alietayari kujibebeza kurithi madeni asiyotabirika lini yatakwisha. Marekani, UK na france ni mfano wa nchi chache tu ambazo ambazo wameweka miguu juu wanajikusanyia mamilioni ya dola kutoka Tanzania bila ya kuvuja josho kupitia IMF na world bank.

Kuna nini zanzibar kitakacho wafanya waarabu kutaka kurudi zanzibar? Uchumi ambao ulikuwa ndio uti wa mgongo wa serikali ya zanzibar umekufa, kila ambacho tunajiringia sasa aidha tumeridhi kutoka kwa utawala waliopita au tumepewa misaada kutoka kwa hao hao tunaowaita wakoloni na masultani.

Mifano ni mingi tu lakini ukianzia hospitali, skuli, college na chuo kikuu vyote vinajengwa au vimejengwa kwa misaada ya nchi za nje. Majengo tuliyorithi ya mji mkongwe kila siku yanaporomoka kwa sababu serikali inashindwa kuyatunza, sio yale waliopewa wananchi waishi bali hata ambayo serikali iliamua kuyafanya wizara za serikali. Wamejikalia tu na kuyatumia bila ya kuyatunza na yanapoporomoka wanawakimbilia waarabu wawasaidie kuyajenga tena. Mfano mzuri wa karibu ni jumba la beit al ajaib, nani analikarabati hivi sasa? Halafu anatoka mtoto wa Karume kuwatukana wafadhili wetu.

Mjini tulirithi system nzuri ya maji safi katika majumba yote, serikali miaka yote hii imeshindwa kudumisha au kuimarisha system hii na sasa mifereji (mabomba kwa lugha ya bara) inatowa maji ya chumvi badala ya maji safi yasio na chumvi. Sitaki hata kugusia drainage system ambayo hadi leo ni ile ile tuliyorithi kwa wakoloni na masultani.

Sina haja hata ya kulia juu ya standard ya elimu nchini, maana imeshagonga chini hata huwezi kusema imeshuka, tatizo ambalo limepelekea kuwepo na kizazi kisichokuwa na elimu, kisichoajirika ambao wanabaki kukaa vibarazani wakitegemea misaada ya ndugu zao walioweza kwenda nchi za wakoloni na masultani kufanya kazi.

Bora nisite hapa, lakini kabla ya kusita nasema hivi Zanzibar kwa sasa tunajisifia kwa kuwa kituo rasmi cha kuingiza madawa ya kulevya afrika, tuna idadi kubwa ya wabugia unga, wizi na wabakaji. Umasikini umekithiri na hulka za kizanzibari zimepotea, na hakuna nchi ambayo iko tayari kuivamia zanzibar, hata wataliana ambao ndio waingizaji wetu wakuu wa madawa ya kulevya hawako tayari kuimiliki nchi hii.

Watanzania na wazanzibari tuamke, hakuna mkoloni, sultani au adui wa nje ya nchi, adui tunae miongoni mwetu.
 
Dk. Mwinyi ahukumiwe kwa vigezo si nasaba

Na Joe Beda

Wanasema Zanzibar ikipiga chafya, mrima kote tunapata homa. Ndiyo hali halisi unayoweza kuieleza kuhusu mchuano wa kutafuta Rais mpya wa visiwa hivyo atakaye hukia nafasi ya Dk. Ali Mohamed Shein.

Wakati naandika makala haya, tayari vikao vy juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) vinakaa kufanya mchujo wa wagombea ili hatimaye apatikane mmoja kutoka miongoni mwa walioomba kupewa nafasi hiyo.

Mwaka huu, idadi ya walioomba nafasi hiyo imekuwa kubwa kuliko kawaida. Zaidi ya watu 30 wameomba ridhaa na kazi itakuwa kupata majina machache kwa ajili ya kufikishwa kwenye vikao vya maamuzi vya chama hicho tawala.

Mshindi wa mchakato huo atapambanishwa na mgombea wa Chama Cha ACT Wazalendo, Seif Shariff Hamad, ambaye ni mkongwe wa siasa za visiwani.

Jambo moja kubwa ambalo halijanivutia kwenye siasa za Zanzibar - hasa hizi za kutafuta kupitishwa na CCM, ni ubaguzi wa wazi ulioonyeshwa dhidi ya baadhi ya wagombea.

Katiba ya Tanzania na ile ya CCM zimesisitiza sana kuhusu haki ya kila mtu kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi ali mradi ana sifa zinazokubalika.

Ni ajabu kwamba wapo wanasiasa wanaotumia vyombo vya habari rasmi na mitandao ya kijamii kuchafua wenzao kisiasa.

Nimeona maneno makali yakiandikwa au kutamkwa kueleza kwanini Wazanzibari hawapaswi kuwachagua watoto wa waliowahi kuwa Marais wa zamani wa Zanzibar.

Walengwa wakuu katika shutuma hizo ni Waziri wa Ulinzi, Dk. Hussein Mwinyi na mwanasiasa mwandamizi, Ali Karume.

Ali ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Zanzibar wakati Mwinyi ni mtoto wa Rais wa Pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi. Wote ni watu wazima waliopita umri wa miaka 50.

Hussein Mwinyi ni mwanasiasa mzoefu. Amekuwa waziri na mbunge kwa takribani miaka 20. Amekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM kwa takribani miaka 10.

Katika miaka ya karibuni, hakuna mwanasiasa wa CCM aliyeomba ridhaa akiwa na wasifu unaofanana na huu.

Baba wa Hussein, Ali Hassan Mwinyi, alikuwa Rais wa Zanzibar akiwa na uzoefu wa chini ya miaka kumi kama waziri. Aboud Jumbe naye hivyo hivyo.

Ali Karume ni mkubwa kiumri zaidi ya Hussein lakini amefanya kazi za kibalozi na kiserikali karibu miaka yake yote ya utu uzima.

Mtu yeyote mwenye wasifu kama wa Hussein na Ali - kuondoa majina ya baba zao, wangeweza kufikiriwa kwa Urais Bara au Visiwani.

Itakuwa ni ubaguzi wa aina yake kumnyima Mwinyi au Ali nafasi eti kwa sababu baba zao waliwahi kuwa Marais.

Hakuna mtu anayechagua baba wa kumzaa. Akina Mwinyi kuwa watoto wa Mzee Ruksa hawakuomba kwa Mungu.

Zanzibar kutanoga zaidi wakati wagombea na wapambe wao watakapoamua kujikita kwenye vigezo vya Rais wamtakaye kuliko kuangalia vinasaba.

Kama wewe una mgombea, mwambie ajitahidi kuzungumza mazuri yake na watu tumkubali au kutokumbali.

Kuna wagombea kama Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, Balozi Nassor Selemani, Shamsi Vuai Nahodha, Masauni Yusuf na wengine wengi wana wasifu wa kutosha kabisa kueleze.

Kila nikiona kinachoendelea Zanzibar; kumbukumbu zinasogea huku Bara kwa vijana wawili; Makongoro Nyerere na Ridhiwani Kikwete.

Leo mmoja wao akitaka Urais wa Tanzania, tutawanyima eti kwa sababu Jakaya na Mwalimu walishawahi kuwa marais na watoto wao hawafai kwa ajili hiyo.

CCM na Wazanzibari wanatakuwa wameruka kikunzi kikubwa kabisa kama wataamua kwamba jambo la muhimu zote litakuwa ni kutafuta kiongozi mwenye maono na atakayeweza kuibadili Zanzibar.

Wakiisha wagombea hao wanaobaguliwa kwa nasaba, utaingia ubaguzi mwingine. Labda kuhusu wa Unguja na Pemba au wa kuja na wazaliwa.

Kama alivyopata kuasa Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu. Anayeanza hawezi kuacha.

Kwa wanaojua ubaya wa ubaguzi au kubaguliwa, hili ni jambo baya sana. Na kwa kisiwa kama Zanzibar, tabia hii ya kubaguana ikianza ndiyo utakuwa mwanzo wa matatizo makubwa ambayo utatuzi wake utachukua muda mrefu.

Zanzibar ina makovu inayotakiwa kuyatibu. Haina sababu ya kuongeza vidonda vingine. Hili limo ndani ya Wazanzibari wenyewe.

Sifa na uwezo wa kupambana na changamoto za sasa za Zanzibar ndiyo inatakiwa kuwa taa ya kuamua nani hatimaye apewe nafasi na jukumu la kupeperusha bendera ya CCM mwaka huu.

Zaidi ya yote, ni kuangalia ni mgombea gani ataisaidia CCM kushinda uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Kwenye Uchaguzi wa mwaka 2015, CCM iliamua kuchagua mgombea atakayekipa ushindi chama dhidi ya vuguvugu la Ukawa. Chama kikaona ni John Pombe Magufuli pekee ambaye angeweza kukivusha.

Kwa Zanzibar, inatakiwa pia kipate mgombea mzuri atakayekipa ushindi dhidi ya Maalim Seif na ACT Wazalendo yake.

Wasiangalie sura wala majina ya ubini. Kama mtu huyu ni Mauldine Castico, apewe nafasi. Kama mtu huyo ni Mbarawa, Mwinyi au Karume; apewe anachostahili.

Kila la kheri kutoka kwa Lyamba la Mfipa.

Mwisho C&P
 
Wewe nani mpaka umweke? Ila watu wa nchi hii kila mtu ana sharubu acha vyombo husika waamue
 
Inachekesha sana. Nchi ni Zanzibar lakini nukuu zinafanywa kutoka kwenye katiba ya JMT.

Katiba ya Zanzibar hakuna???
 
Naomba ateuliwe Mbarawa. ili hasira zisababishe kura nyingi kwa Seif Maalim
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…