Bara la Afrika ukilichimba kwa ndani limetapakaa utajiri tu, mabeberu wanatamani tubadilishane mabara

Bara la Afrika ukilichimba kwa ndani limetapakaa utajiri tu, mabeberu wanatamani tubadilishane mabara

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,840
Reaction score
8,202

Wanakijiji walivyokimbilia kuchimba dhahabu iliyopatikana karibu na zizi la ng'ombe​

Watu wakichimba dhahabu eneo la  Springs, Afrika Kusini


Watu wengi wamekimbilia kuchimba dhahabu katika eneo la makazi duni mashariki mwa mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, baada ya tangazo kutolewa siku chache zilizopita kuwa kuna dhahabu eneo hilo.
Mwanamke anaonyesha  maumivu wakati mwanamke mwingine akimsaidia kupakia mfuko wa udongo kwenye bega lake


Mkaazi mmoja wa eneo hilo lililoko karibu na eneo la migodi la Springs alisema alipata chembe chembe za dhahabu akiwa analima karibu na zizi la ngombe.
Makumi ya watu sasa wamehamia eneo hilo wakichimba karibu na zizi la ngombe wakiwa na matuamaini ya kutajirika.
Mwanamke anatumia sepeto kujaza ndoo na udongo karibu na watoto wake huku wachimbaji wengine  wakichimba mashimo wakitafuta dhahabu katika kipande cha ardhi nje ya Springs.


Wakiwa wamejihami na mapanga na majembe, wamekuwa wakichambua udongo katika eneo linalofanana na eneo la awali Afrika Kusini ilichimba dhahabu na kujitajirisha mwongo mmoja uliopita.
Eneo la Springs hapo awali ilikuwa mji wa dhahabu na wenye shughuli nyingi, lakini migodi yake ilifungwa miaka kadhaa iliyopita kwa sababu kina cha mashimo yalikuwa ndefu sana na hatari.
Watu wengine waliambia BBC walipata dhahabu


Idara ya madini Afrika Kusini, imekosoa vikali uchimbaji uliofanyika wiki hii katika makaazi ya Springs eneo la Gugulethu, na kusema ni kinyume cha sheria kwani inaharibu mazingira.
Mtu anatumia sahani kuangalia  chembe chembe ndogo za dhahabu.


Baadhi ya wale waliokuwa wakichimba dhahabu eneo hilo wameiambia BBC kuwa waliweza kupata dhahabu na kuuza katika soko zisizo rasmi.
Kemikali hatari kama Zenaki na sodium cyanide zinatumika ili kutenganisha dhahabu na mawe.
 
Kuna hadithi inasimuliwa kwamba fisi alikufa na njaa akiwa kwenye shamba la miwa asijue kwamba alikuwa amezungukwa na chakula.
 
Back
Top Bottom