Barabara 3 zenye urefu wa Kilometa 238.9 zimejengwa kwa Tsh. Bilioni 321.24 Mkoani Tabora

Barabara 3 zenye urefu wa Kilometa 238.9 zimejengwa kwa Tsh. Bilioni 321.24 Mkoani Tabora

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Tabora ni moja ya miji ambayo Serikali ya Tanzania imewekeza nguvu katika kuboresha miundombinu ya barabara ambapo kuna miradi kadhaa inaendelea na mingine imekamilika.

Rwegoshora Michael ambaye ni Kaimu Meneja wa TANROADS Tabora, ameeleza kuwa kwa jumla mkoa huo una Kilometa 2,188.09 za barabara ambazo zinahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Ameeleza kuwa kati ya hizo Kilometa hizo, 967.09 ni za barabara kuu na 1158.01 ni barabara za Mkoa zikiwemo 62.99 za ngazi ya Wilaya.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo, amesema Kilometa 794.67 ni barabara kuu pia za kiwango cha lami ni Kilometa 1172.42, barabara za mkoa ni Kilometa53.74 ambazo ni lami na Kilometa 1104.27 ni za udongo wakati Kilometa 62.99 ni barabara za Wilaya.

Upande wa madaraja, ameweka wazi kuwa mkoa una hudumia madaraja 596 yaliyojengwa kwenye mtandao huo unaosimamiwa na TANROADS.

MIRADI YA MAENDELEO: Mhandisi Rwegoshora amesema jumla ya Kilometa 238.9 zimejengwa kwa kiasi cha Tsh. Bilioni 321.24 mkoani hapo, pia ameweka wazi mradi mmoja unatakelezwa na upo katika wastani wa kiwango cha 89.62%.

Baadhi ya miradi iliyotekelezwa Mkoani Tabora ni ujenzi wa Barabara ya Tabora – Mpanda kwa kiwango cha lami Kilometa 117.5 ambayo imegharimu Tsh. Bilioni 165 na imetekelezwa kwa kiwango cha 100%.

Mradi mwingine ni ujenzi wa Barabara ya Kazilambwa - Chagu kwa kiwango cha lami kwa Kilometa 36 ambapo umegharimu Tsh. Bilioni 38.307, wenyewe upo kwenye kiwango cha 89.62%

Mhandisi Rwegoshora ameweka wazi kuwa Mradi huo unatarajiwa kumalizika Juni 30, 2023, upo kwenye barabara kuu.

Kuhusu sehemu ya faida ya mradi huo ni kuwezesha usafirishaji wa abiria na mizigo, kurahisishwa usafiri wa wananchi wa Kigoma na kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa kipande ambacho kilikuwa kimebaki.

SHUKRANI KWA SERIKALI: Amesema: “TANROADS Tabora tunaishukuru Serikali ya Awamu ya 6 kwa kutuletea mradi huu, pia kwa juhudi kubwa zinazofanywa kuhakikisha malipo kwa wakandarasi kwa wakati.”

Mradi wa tatu ni ujenzi wa Barabara ya Nyaua – Chaya wenye urefu wa Kilometa 85.4 kwa kiwango cha lami ukiwa umegharimu Tsh. Bilioni 117.939 na umekamilika kwa 100%.

Upande wa Injinia Joseph Isaya Mosha ambaye ni Mhandisi Mshauri katika mradi wa Kazilambwa-Chagu amesema kati ya Kilometa 36, Kilometa 26 zipo upande wa Tabora na 10 nyingine zipo upande wa Kigoma zote zinaendelea katika hatua nzuri ya utekelezaji.

Mhandisi Rwegoshora amesisitiza “Tunafurahi kuona tunaelekea mwishoni, pia tunashirikiana vizuri na TANROADS katika kusimamia kazi anazofanya Mkandarasi, zinafanyika katika kiwango stahiki.

“Manufaa ya mradi huu hapa kuna ajira zaidi ya 400 zilizotolewa na mkandarasi na asilimia kubwa zinawalenga wazawa, pia kuna ajira ambazo si za moja kwa moja zinazotokana na watu kujiajiri kufanya biashara kwa waajiriwa wa mradi na watu wengine.

“Mkandarasi pia amesaidia katika huduma za jamii hasa upande wa upatikanaji wa maji kwa kuchimba visima ambavyo pia vinatumiwa na jamii.”
 
Ilianza Moro, ikaja Dodoma na sasa ni tabora. Ila Tabora ripot kuisoma hata haieleweki hivi.

Watudanganye na mapicha picha maana wa Dom wamekuja na video za wananchi wakifurahia ujenzi.
 
Back
Top Bottom