KERO Barabara iliyojengwa Keko ni ya kupita gari moja tu, gari likiharibika itakuwaje?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Sasa Kama haipitishi magari hata mawili Kuna haja gani ya kujenga. Bora ilivyokuwa mwanzo

Ilivyokuwa mwanzo si hakukuwa na BRT mkuu, maana yake ni kuwa BRT imechukua nafasi ya iliyokuwa barabara ya lami mwanzo

Kama ilivyo barabara ya Msimbazi K'koo, hawakuweza dondosha magorofa yale, ikabidi tu waweke njia moja ya lami kila upande, na waboreshe njia za ndani kwa ndani ziwe michepuko...
 
Ujenzi wa barabara za mwendokasi BRT kwa kutumia mabasi haukuwa uamuzi wa busara. Hizi njia za mwendokasi zingewekwa reli ili trams🚊🚃 zitumike badała ya mabasi. Hii ingekuwa kama kuua ndege wengi kwa jiwe moja, lakini tram iliyounganisha mabehewa matatu hadi manne ingebeba abiria wengi kwa wakati mmoja.
 
Umeona zile kingo, ya msimbazi kingo ni fupi, gari ikiharibika inaweza sogezwa kwenye njia ya mwendokasi, pale no
 
Kama hamna picha ni uzandiki wa kawaida kabisa
 
Hata Mimi ile barabara huwa inanipa maswali mengi sana kama hayo

Kitu Cha kushangaza barabara ya mwendokasi ndio imepewa eneo kubwa sana wakati ingewezekana kuibana na kuongeza hizi barabara za pembeni
 
Hata Mimi ile barabara huwa inanipa maswali mengi sana kama hayo

Kitu Cha kushangaza barabara ya mwendokasi ndio imepewa eneo kubwa sana wakati ingewezekana kuibana na kuongeza hizi barabara za pembeni
Ni balaa, sijui tunaenda mbele, au tunarudi nyuma
 
...Usiseme gari likiharibika TU! Je Magari yanapishana Kawaida ama Barabara ni Nyembamba mno Hata hayawezi Kupishana???
 
Picha iko wapi?
 
Gari moja inapitaje?
Imekuwa kama parking za kwenye nyumba.
 
Waliochukua nchi baada ya Uhuru hawakufanya la maana zaidi ya kukuza kiswahili...

Hawakujihusisha kabisa na upangaji wa miji, hadi leo Awamu ya 6 bado miji yetu haipangwi
 
Wazee wa kubomoa lipa fidia jenga
Kujenga kwenyewe magumashi
Bomoa jenga bomoa jenga

Ova
 
Habari bila picha/video clip sawa na takataka tu. Dunia y sasa au majungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…