Barabara kuu Dar-Lindi imekatika sehemu 2 na kukata mawasilino

Barabara kuu Dar-Lindi imekatika sehemu 2 na kukata mawasilino

gubegubekubwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2008
Posts
668
Reaction score
898
Barabara ya Dar es Salaam-Lindi imekatika eneo la somanga na kukata mawasilino kabisa kati ya Dar na Lindi hivyo hamna gari lolote la kwenda Lindi au Kwenda Dar. Kwasasa abilia na wote wenye magari tupo hapa tumekwama tangu Jana. Tunaomba Tanroads walishughurikie haraka hili.

1714910252690.png

Chadema watakwambia shida ni kukosa Katiba Mpya 😂😂
 
Maji hayajawahi kushindwa asee, hapo waweke daraja la muda la jeshi
 
Barabara ya Dar es Salaam-Lindi imekatika eneo la somanga na kukata mawasilino kabisa kati ya Dar na Lindi hivyo hamna gari lolote la kwenda Lindi au Kwenda Dar. Kwasasa abilia na wote wenye magari tupo hapa tumekwama tangu Jana. Tunaomba Tanroads walishughurikie haraka hili.

Hapo chini hiko ni kifusi wacholiweka wakati wanatengeneza ni udongo wa shambani au? .halafu ujazo wa lami mbona mdogo sana...wakandarasi wa barabara zetu ni wezi wezi...
 
TANROAD LINDI watoa hali halisi ilivyo Somanga Mtama Pwani asubuhi tarehe 5 May 2024 akiongea jinsi tuta lilivyoliwa na maji

View: https://m.youtube.com/watch?v=HEsXqeLNeto

Kwa mujibu wa meneja wa TANROADS mkoa wa Lindi, Mhandishi Emil Zengo kimbunga Hidaya kimechangia kusukuma maji kwa wingi na maji yaho yamefanya uharibifu kwenye barabara ya Somanga – Mtama na kukata tuta la barabara hiyo eneo la Mikereng'ende umbali wa Kilomita 10 kutokea Somanga uelekeo wa Lindi.

Nangurukuru mto nako umekula barabara Lindi hivyo waendesha vyombo vya barabarani wawe wastahimilivu na wafuatilie TANROADS HQ instagram na wa wizara Ujenzi
 
TOKA

TOKA MAKTABA:​

March 6, 2024​

Bashungwa amsimamisha kazi Meneja Tanroads Lindi​

Shununa Haji March 6, 2024
BASHIIIII-780x470.jpg
Picha maktaba : Waziri Innocent Bashungwa

LINDI: WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi Meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi, Mhandisi Andrea Kasamwa kwa kushindwa kusimamia urejeshwaji wa miundombinu ya barabara na madaraja katika Wilaya ya Liwale mkoani Lindi na kusababisha barabara kuu zinanounganisha wilaya hiyo na maeneo mengine kufungwa.

Pia Waziri Bashungwa akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Deo Ndejembi ameshuhudia urejeshwaji wa barabara ya Liwale – Nangurukuru iliyosombwa na maji ikisimamiwa na mtaalam mwenye taaluma ya Falsafa kwa kusaidiwa na wananchi wakati mkandarasi akiwa hayupo eneo la kazi.

Waziri Bashungwa amechukua hatua hiyo leo Machi 6, 2024 wakati akikagua mindombinu ya barabara katika Wilaya ya Liwale na kutoridhishwa na usimamizi wa kazi inayofanywa na Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Lindi.

“Haiwezekani sisi tutoke Dodoma hadi huku Liwale kutokana na changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara iliyopo, Mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan amelazimika kutoa helikopta yake tufike huku, lakini hapa site hakuna Mkandarasi, mnaweka mtu aliyesoma falsafa kusimamia kazi ya ujenzi wa barabara,” amesema Bashungwa.

Amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta, kupeleka wataalam na kuhakikisha ndani ya siku nne barabara zote kuu na madaraja yanayounganisha Wilaya ya Liwale na maeneo mengine katika mkoa huo ambayo hayapitiki yawe yamefunguliwa na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi
 
Mkuu hakuna anaeweza kukadiria mafuriko. Hii ni dunia nzima. Hizi sio mvua za kawaida ni mafuriko popote duniani hakuna anaeweza kuzuia.
Kuna maeneo yenye historia ya mafuriko. Mkandarasi anatakiwa kujua. Unataka kuniambia jangwani pale RBT hawakujua kuwa ni mkondo wa maji?
 
Barabara ya Dar es Salaam-Lindi imekatika eneo la somanga na kukata mawasilino kabisa kati ya Dar na Lindi hivyo hamna gari lolote la kwenda Lindi au Kwenda Dar. Kwasasa abilia na wote wenye magari tupo hapa tumekwama tangu Jana. Tunaomba Tanroads walishughurikie haraka hili.

Poleni Sana
 
Back
Top Bottom