gubegubekubwa
JF-Expert Member
- Jun 9, 2008
- 668
- 898
Barabara ya Dar es Salaam-Lindi imekatika eneo la somanga na kukata mawasilino kabisa kati ya Dar na Lindi hivyo hamna gari lolote la kwenda Lindi au Kwenda Dar. Kwasasa abilia na wote wenye magari tupo hapa tumekwama tangu Jana. Tunaomba Tanroads walishughurikie haraka hili.
====
Serikali imewatoa hofu abiria wanaosafiri kutoka Dar es salaam kwenda Mikoa ya Lindi na Mtwara na wale wanaokuja Dar es salaam ambao wamekwama baada ya barabara ya Dar es salaam - Lindi kuharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zikiambatana na kimbunga Hidaya ambapo imesema tayari TANROADS inapambana kurejesha mawasiliano.
Mapema leo asubuhi maji yamefurika kwa wingi na kuharibu eneo la takribani mita 80 katika barabara ya Somanga – Mtama na kukata tuta la barabara hiyo eneo la Mikereng’ende umbali wa Kilomita 10 kutokea Somanga uelekeo wa Lindi na pia imeleta athari katika eneo la Lingaula umbali wa kilomita 12 kutokea Nangurukulu uelekeo wa Lindi.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi Emil Zengo ametembelea eneo hilo na kukagua uharibifu uliotokea akiwa na Timu ya TANROADS na Wakandarasi ambapo wanaendelea na kazi ya kurejesha miundombinu.
Amesema jitihada za Serikali zinaendelea kufanywa ili kurejesha mawasiliano ya barabara hiyo kutokea upande wa Mkoa Pwani na kutokea Lindi huku akitoa wito kwa Wananchi na Madereva kuendelea kuwa na subira kwani Serikali kupitia TANROADS inaendelea kufanya kila linalowezekana kurejesha miundombinu ya barabara hiyo na kuwezesha Wananchi kupata huduma ya usafiri katika barabara kama kawaida.
Chanzo: Millard Ayo
Maagizo ya Waziri - Waziri wa Ujenzi atoa maelekezo mawasiliano Barabara ya Dar - Lingi yarejee ndani ya Saa 72