KERO Responded Barabara mbovu sana kiwanda cha Namela njia ya Ulongoni

KERO Responded Barabara mbovu sana kiwanda cha Namela njia ya Ulongoni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Malaki

Member
Joined
Jan 12, 2016
Posts
87
Reaction score
42
Njia ya kuingia kutoka G/mboto kwenda ulingoni kwa Gari ni njia moja tu ambayo hiyo ndo inategemewa na magari makubwa na daladala za kwenda kinyerezi, mbezi.Hii barabara mbovu sana na imekua hivo kwa muda wa miaka 3 sasa na toka walivoondoka wakandarasi waliokua wanajenga reli ya SGR Pale pugu mpaka leo hali ni tete.

Chaa ajabu ile barabara yanapita magari makubwa sana kwa sasa yanachimba mchanga mto msimbazi kwa muda wa miezi 6 nayaona.Pale mtoni hayo magari yanaharibu barabara na pia hatujua ni ya maradi gani au biashara ya mtu na mto upande mchanga unapotoka pamebomoka tayari inamana ni hatari sana kwa baadae.
Serikali za mtaa,madiwani na wajumbe wa mitaa pale ulongoni,G/mboto wapo muda wote huu miaka inasogea na kile ni kipande kidogo sana kama km1.2.

Kuna mradi wa mwendo kasi upande wa G/mboto barabara kubwa ambapo pamepakana na kuna kifusi kingi ambacho mimi mwenyewe niliuliza kuwa kama kina kazi wakasem hiki huwa wanatumia kama watakihitaji, lakini sio muhimu kwao nikaomba nikapewa gari moja,kwaajili ha mahitaji yangu binafsi.

Nauliza Serikali kama magari ya abiria yameanza kupita hizi Serikali za mtaa
1. Wajumbe

2. Serikali za mitaa

3. Madiwani

4. Mbunge wetu

Maana hii njia ya magari yanayoenda mnadani na magari yanabeba ng'ombe pia hizo daladala zinapita kila siku, naomba Serikali na jamii ya

1. Ulongoni A
2. Ulongoni B
3. G/mboto
4. Kinyerezi

Wakae watatue matatizo ya wananchi watazidisha tatizo pale mto msimbazi na hapana hata miaka 5 toka pamekamilika lile daraja la Ulongoni B.


Pendekezo
Waombe kifusi kutoka jirani pale mradi wa mwendokasi na vifaa ndani ya muda wa masaa 2 ile kazi inakamilika ni
1. Kuchimba mtaro na

2. Kufukia mashimbo na kuisawazisha

Hii kero ya muda inafumbiwa macho hadi mbunge sehemu kama ile yenye manufaa ya mnadani na njia Ulongoni, Kinyerezi na Gongo la mboto pamoja na kiwanda cha Namera kiwajibishwe kwa kukosa kutoa taarifa.
 
Mbona kutoka Namera Group Kuna lami had kinyerezi huko na bajaji zinapita au Unaongelea Barabara ya Pugu mnadani
 
Wametengeneza tayari


20240508_064256.jpg
 
Back
Top Bottom