Barabara mpya na za kisasa kwenye miji mikubwa ni kwa ajili ya kupendezesha miji?

Barabara mpya na za kisasa kwenye miji mikubwa ni kwa ajili ya kupendezesha miji?

Kecha Boksi

Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
55
Reaction score
109
Wasalaam,

Hizi barabara mpya na za kisasa za kuingia kwenye miji yetu mikubwa ni kwa ajili ya kupendezesha miji?

Fikiria barabara kubwa ya kuingia mji mkubwa wa kibiashara Tanzania? Njia nne kwenda njia nne kurudi. Anzia Kimara mwisho hadi inapoishia ni vibao vya hamsini mwanzo mwisho. Kila mita chache kibao cha hamsini na trafiki waliojificha wengi vibao vinapoishia.

Madereva kwenye barabara hii wanateseka sana. Wanatembea kwa mateso sana kwenye hii barabara. Wakizidisha spidi ya hamsini ni tozo ama kubrashi viatu kwa kwenda mbele.

Haya tuseme hii ya kuingia jiji la Makala haijaisha na haijakabidhiwa. Twende Chuga. Barabara mpya na ya kisasa toka Tengeru hadi town. Mandhari yamependeza.

Ila kuta madereva walivyo waoga barabara hii? Kila kona vibao vya hamsini. Zidisha ulipe tozo ama ubrashi viatu. Yaani Tengeru hadi town Arusha ni kipande kigumu sana kwa madereva.

Sawa, kuna watumiaji wengine wa barabara. Waenda kwa miguu na wengineo. Ina maana hii miradi mikubwa ya mabarabara imeshindwa kutambua haya? Kwanini hawakuweka vivuko vya waenda kwa miguu ili madereva waache hofu? Mbona kwingine wamefanya hivi kwenye barabara zao na kila mtu ana amani?

Hao wanaofanya upembuzi yakinifu na usanifu miradi hii ya barabara ni trafiki ili wapate tozo na kubrashi viatu? Ama lengo kuu ni kutoa na kuingiza magari na watumiaji wengine kwa usanifu kwenye miji yetu?

Aagh..naomba nikachote maji nasikia yameanza kutoka.
 
Hakuna kitu huwa kinauma kama hizo faini, mimi barabarani nakuwaga mpole tu cha maana nifike salama.
 
Point, unakuta ni highway hakuna wakatisha kwa miguu( na kama wapo kwenye highway inabidi wawekewe crossing bridges) ila bado unakuta watu wamejificha na matochi na vibao vya 50 kila hatua 200. Nchi hizi za kiafrika ni ngumu sana!!!
 
lengo la serikali ni kurudisha gharama zao walizotumia kujenga hiyo miundombinu(faini kwa trafick)
 
Point muhimu. Na pia kuna vyanzo vizuri tu vya mapato ambavyo wala hawaviangalii. Kwa mfano, kila siku asubuhi na jioni katika vituo vya daladala, nimegundua bajaji, bodaboda na wakati mwingine magari ya biashara zingine (mfano ya matangazo) yanapaki katika vituo hivyo. Hali hii inaongeza sana misongamano na kusababisha foleni. Waelekeze nguvu huko.

Highways inatakiwa magari yaende kwa kasi zaidi (speed limit iwe juu zaidi) hivi hivi tunakuwa tumepoteza tu pesa za walipa kodi kwa kujenga hizi barabara.
 
Back
Top Bottom