KERO Barabara Mtaa wa Magomeni Jitini - Unguja, imechimbwa na kutelekezwa, kuna usumbufu mkubwa wa magari kupishana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Hapa Mtaani kwetu Magomeni Jitini katika Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja tuna kero ambayo imekuwa ikitusumbua kwa muda wa wiki tatu sasa.

Kuna Barabara imechimbwa, hakuna ujenzi unaoendelea mpaka sasa, hali inayofanya madereva kutumia njia moja hali inayosababisha kero ya foleni na usumbufu mwingine wakati wa kupita.

Wanaohusika na ujenzi huu wajue wanatutesa, waje wamalizie kilichowafanya wachimbe eneo hilo, ni kero kubwa.
photo_2024-11-26_15-47-41.jpg

photo_2024-11-26_15-47-40.jpg

photo_2024-11-26_15-47-38.jpg

photo_2024-11-26_15-47-28.jpg
 
Mbona unguja tunaambiwa ni kama Dubai tu, sasa hayo mandhari yanatoka wapi tena.

CCM ni ileile tu, Iwe Zanzibar Island au Tanganyika.
 
Hapa Mtaani kwetu Magomeni Jitini katika Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja tuna kero ambayo imekuwa ikitusumbua kwa muda wa wiki tatu sasa.

Kuna Barabara imechimbwa, hakuna ujenzi unaoendelea mpaka sasa, hali inayofanya madereva kutumia njia moja hali inayosababisha kero ya foleni na usumbufu mwingine wakati wa kupita.

Wanaohusika na ujenzi huu wajue wanatutesa, waje wamalizie kilichowafanya wachimbe eneo hilo, ni kero kubwa.
Pitia amani au mazizini kama unaenda fuoni. njia safi kabisa. Allah awajaalie viongozi wae na hekima zaidi
 
Back
Top Bottom