Hapa Mtaani kwetu Magomeni Jitini katika Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja tuna kero ambayo imekuwa ikitusumbua kwa muda wa wiki tatu sasa.
Kuna Barabara imechimbwa, hakuna ujenzi unaoendelea mpaka sasa, hali inayofanya madereva kutumia njia moja hali inayosababisha kero ya foleni na usumbufu mwingine wakati wa kupita.
Wanaohusika na ujenzi huu wajue wanatutesa, waje wamalizie kilichowafanya wachimbe eneo hilo, ni kero kubwa.