Barabara ya Geita kwenda Kamyorwa itengenezwe upya,ni kiungo muhimu kwa uchumi wa taifa

Barabara ya Geita kwenda Kamyorwa itengenezwe upya,ni kiungo muhimu kwa uchumi wa taifa

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Kwa wakazi wa mikoa ya Mwanza,Geita na Kagera wanafahamu umuhimu wa hii barabara hasa kwa uchumi wa eneo hili. Maana ni njia muhimu sana katika kusafirisha watu na bidhaa hasa kwa eneo hili.

Hii barabara ilikamilika mwaka 2008 na hapo ndipo ilichochea maendeleo hasa sehemu ilizopita.

Kabla ya ujenzi wake ilichukua takribani masaaa kumi kufika Kagera ukitokea Mwanza. Lakini ilipokamiliia ni masaa matano mpaka sita.

Ifahamike life spam ya barabara ya lami huwa ni miaka kumi na kwa sasa imefikisha miaka tisa imeshachoka.

Sababu hii inatakiwa itengenezwe upya na sio kama mara ya kwanza ambapo ilikuwa ni lami ya class 1 bali iwe class 3 ili ubora uongezeke.

Hivyo serikali ilifanyie kazi ombi hili kwa manufaa ya wananchi wa mikoa ya Kanda ya ziwa na taifa kwa ujumla.
 
Nchi ya kwenu hii wasukuma msiwe na wasiwasi kila barabara ya itawekwa lami
 
Back
Top Bottom