Barabara ya Igawa-Mbeya, inajirudia kuwa a Hell Run!

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839


Barabara hii ya Igawa-Mbeya hadi Tunduma, imeanza kurudi zama zake miaka ya 60, ikiitwa The Hell Run. Kwa sasa safiri barabara hii at your own risk, barabara ni mbaya kuliko.

Mida ya saa 8 usiku, nimepata double puncture baada ya kuingia shimo kisawasawa.
 
Kwa nini hii barabara hwakumaliza kuijenga hadi Tunduma?
 
Hiyo TanZam Highway ni mtihani sana nilisikia walianza kujenga njia nne imeishia wapi, kuna kipande kingine kiko Iwambi pale na chenyewe kimesumbua sana malori yalikuwa yanaanguka karibu kila siku sijui kama wamerekebisha, Mbeya pamesahaulika sana kimiundombinu asee
 
Kwa nini hii barabara hwakumaliza kuijenga hadi Tunduma?
Barabara hii inatakiwa ijengwe kwa zege kutokana na uzito na wingi wa magari.
Ufisadi wa viongozi wa CCM ndiyo chanzo kujengwa kila mara huku wao wakitajirika. Miaka ya sabini serikali ilitumia pesa nyingi sana kujenga reli ya Tazara ili ibebe mizigo yote ipelekwayo nyanda za juu kusini na nchi jirani za Malawi, Zambia, Zimbabwe na Kongo, viongozi wa CCM wamekuwa wakiihujumu Tazara mpaka imemekufa huku wakipeleka matrilioni kila mwezi kukarabati barabara hii inayoanzia Dar es Salaam! Ni umbali mrefu sana, hii yote ni kwa sababu magari yao yanapita kupeleka mizigo kusini mwa Tanzania huku reli ya Tazara ikokosa mizigo!
Wakati umefika kwa watanzania kusema sasa imetosha na kutaka magari mazito ya mizigo yashushe mizigo Tunduma ipelekwe Dar es Salaam kwa treni.
 
Mimi pia nilishapata pancha mitaa hiyo. Nikiwa na Toyota Crown tairi law profile la nyuma. Ilikuwa mwaka juzi mwezi wa 12.
 
Mkuu Ukitoka Tunduma Mpaka Ufike Mpakani MwA Mkoa Wa Mbeya Na Njombe
Hapo Ndiyo Utapata Barabara Iliyotulia,


Barabara Nzuri Nzuri Kuanzia Namanyere Kuja Tunduma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…