BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Sisi wakazi wa Igunga ambao tumekuwa tukifanya shughuli zetu kutoka Wilayani hapa kueleke Mbeya tumekuwa tukikutana na changamoto kubwa ua ubovu wa Barabara.
Kwanza kabisa kabla sijaingia katika hoja yangu ya msingi, huku vijiji vyetu vina changamoto kubwa ya Barabara kuingia kwenye vijiji mbalimbali, nyingi ni mbovu na hivyo tunashindwa kuingia na magari pale inapolazimika kuwa hivyo.
Nije katika hoja ya msingi, kumekuwa na mazingira ambayo sijui niyaite ni uzembe wa ukarabati barabara inayounganisha Igunga na Rungwe Mkoani Mbeya.
Barabara hiyo imekuwa haipitiki kabisa kipindi cha masika lakini hata vipande ninavyokarabatiwa huwa havichongewi mitaro, matokeo yake wanasababisha baadhi ya maeneo yanakatika ovyo.
Mvua zikiisha wanakuja kurekebisha kwa kugusagusa, hawaweki mitaro kama nilivyoeleza hapo, ikitokea mvua zimeanza maji yanapokuwa yanasafiri yanaondoka na udongo wa Barabara.
Wakati wa mvua usafiri huwa ni shida kubwa katika njia hii, baadhi ya mabasi yanasimamisha huduma mengine yanalazimika kuzunguka njia ndefu.
Hivi karibuni Desemba 2024 ilifanyiwa marekebisho lakini mwezi mmoja baadaye hali ni kama hivyo unavyoona kwenye picha, Vijiji vingi vinaathirika wakati wa mvua ikiwemo vya Vijiji vya Mwanzugi, Itumba na Muhama.