Nafikiri barabara zote kubwa kama Bagamoyo Road, Kilwa Road, Morogoro Road, Mandela Express, Sam Nujoma jijini Dar es Salaam na barabara za aina hiyo katika majiji ya Mwanza, Mbeya, Iringa n.k hazifai kutumiwa na bajaji, bodaboda kufanya usafirishaji abiria.
Hata zile barabara za kuunganisha mikoa au nchi na nchi vyombo hivi vidogo vopigwe marufuku kutumia highways, barabara kuu. Vyombo hivyo vidogo viruhusiwe kupokea abiria kutoka barabara kuu kuingia mitaani na vijijini tu.
Vyombo hivyo vidogo vipangiwe barabara ndogo za michepuko mitaani lakini barabara kuu ziachiwe malori, mabasi, magari madogo ya binafsi, teksi, mabasi ya mwendokasi na daladala kubwa tu.
Hii ya kulazimisha vyombo vidogo kama bajaji, bodaboda kuingia katika barabara kuu ni hatari na vurugu.