adriz
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 12,207
- 26,521
Moja kwa moja.
Siku za hivi karibuni nilipanda usafiri wa daladala kutoka banana hadi kivule kwenye harakati zangu ,Kwa kweli Ktk Maisha yangu sijawahi shuhudia barabara mbovu kama ile na kila siku hali ile ile miaka nenda miaka rudi
Kutokana na ubovu wa barabara uliopitiliza nilipata changamoto zifuatazo ;
1.Mwili kuuma na maumivu ya kichwa kutoka na gari kurusha na kudunda kwenye mashimo ambayo yapo karibia njia nzima .
2.Masikio kuuma kuliko sababishwa mitikisiko ya mara kwa mara na inayopelekea vyuma na vioo vya gari hutoa sauti ya Kukera kutokana migogano na misuguano .
3.Mafua na kifua hali iliyosababishwa na vumbi njia nzima.
Baada ya gari kufikia mwisho wa kituo abiria karibia wote walihema na kikohoa kama wamemaliza mbio za marathon ,baadhi yao wakawa wanaongea huku wakishuka mmoja akisema "hii njia kama una mjamzito ujauzito unatoka njiani" mwingine nilimnukuu akisema "hii barabara imezidi ubovu kama hatuko dar es salaam"
Mimi binafsi nashangaa sana kwa uongozi wa jimbo la ukonga kutotatua tatizo hili kwa muda mrefu kwani barabara ile muhimu sana kuunganisha wananchi Ktk shughuli mbalimbali za kiuchumi na kufikia maeneo muhimu kama Muhimbil n.k