A
Anonymous
Guest
Barabara ya kutoka Mbezi (Kwa Yusufu) kwenda Mpiji Magoe hadi Bunju imekuwa kama sehemu ya kitega uchumi.
Ipo chini ya TANROADS na serikali ya Magufuli iliweka bajeti ijengwe lakini bajeti hatujui ilienda wapi baada ya kufariki Mzee wetu.
Leo inakarabatiwa kila kukicha(jambo zuri tupate urahisi) lakini bajeti ya kukarabati nadhani mpaka sasa inaweza imepita gharama za kuweka lami mara mbili.
Tatizo ni nini? Tumepiga kelele, wabunge wameahidi miaka nenda rudi. Tukadhani ni kwa sababu ya wabunge wapinzani tulionao lakini leo tuna mbunge CCM, Hadi Rais Magufuli aliahidi.
Je, kuna sababu za kueleweka kwa nini iliahirishwa kujengwa? Na kwa hakuna dalili mpaka leo zaidi tunaona wakarabati wanaweka miundo mbinu ambayo inaashiria hakuna ujenzi kwa miaka ya hivi karibuni?
Tunapata shida kubwa sana.