Mheshimiwa Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, hongera Kwa kazi kubwa unayowafanyia wakazi wa Dar.
Naomba upitie barabara kutokea Magomeni inayopita Tandale Ili iunganishe na barabara ya Shekilango, kuna uharibifu mkubwa wa mazingira. Barabara nzima imegeuzwa dampo ya magari chakavu au gereji.
Kwa kweli uchafuzi huu ni mkubwa ukizingatia pia ni makazi ya watu.
Tunaomba serikali ichukue hatua Ili kunusuru afya za wakazi wa hapo.
Hiyo ndio hospitali ya body za magari, ukiwa na gari yako unataka kuigeuza scrapper uuze peleka hapo, inataka kifaa uhamishie kwenye gari yako nenda pale utakipata, kupaka gari rangi katafute mtaalamu pale....