Barabara ya Mbeya - Mkiwa Kuendelea Kujengwa kwa Awamu

Barabara ya Mbeya - Mkiwa Kuendelea Kujengwa kwa Awamu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

BARABARA YA MBEYA - MKIWA KUENDELEA KUJENGWA KWA AWAMU.

Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema Serikali inajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Mbeya - Chunya - Makongolosi - Rungwa - Mkiwa (km 503.36) kwa awamu ambapo sehemu ya Mbeya - Chunya - Makongolosi (km 111) ujenzi umekamilika.

Eng. Kasekenya amesema hayo Februari 5,2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Lupa Masache Kasaka aliyeuliza ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Makongolosi - Rungwa.

"Ujenzi wa sehemu ya Noranga - Itigi - Mkiwa (km 56.9) sehemu ya Noranga - Itigi (Mlongaji) (km 25.) umefikia asilimia 72 na kwa sehemu ya Noranga - Doroto (km 6) na Itigi - Mkiwa (km 25.6) kazi ya ujenzi zimeanza na utekelezaji wa mradi unaendelea"- amesema Eng. Kasekenya.

Eng. Kasekenya ameongeza kuwa kwa sehemu iliyobaki ya barabara ya Makongolosi - Rungwa Noranga (km 356) Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi.

Kuhusu upanuzi wa Barabara ya Moshi - Arusha eneo la Kikavu, Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema taratibu za manunuzi zinaendelea kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA).
 

Attachments

  • UntitledNBVCX.jpg
    UntitledNBVCX.jpg
    326.7 KB · Views: 7
  • vlcsnap-2023-10-31-22h32m10s437ssa.png
    vlcsnap-2023-10-31-22h32m10s437ssa.png
    107.2 KB · Views: 8
  • GFkBaz8WAAAEGSP.jpg
    GFkBaz8WAAAEGSP.jpg
    61.2 KB · Views: 11
Hii barabara itafanya Mbeya kuwa karibu sana na Kanda ya Ziwa.
 
Jamani hiyo barabara mbona inapita kwenye mapori ya hifadhi? altenatives za Manyoni kwenda Mbeya zipo, shida nini kwenye vipaumbele vyetu?
 
Back
Top Bottom