KERO Responded Barabara ya Mbezi Luis kwenda Mpigi Magoe ni mbovu sana, Wananchi tunateseka jamani

KERO Responded Barabara ya Mbezi Luis kwenda Mpigi Magoe ni mbovu sana, Wananchi tunateseka jamani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mbunge wa huko sijui ni nani, nasikia alihamisha lami kwenda kwake Kibamba badala ya barabara hiyo.
 
Mbunge wa huko sijui ni nani, nasikia alihamisha lami kwenda kwake Kibamba badala ya barabara hiyo.
Hiyo barabara ilikuwa ijengwe kwa lami kuendeleza ile barabara ya Mbezi Kinyerezi. Kilichotokea sasa..... lami imepelekwa Kibamba Chama kwenda Kibwegere.
 
Tukiambiwa tangu mwaka Jana Mwezi wa pili alikua anatafutwa mkandarasi. Mpaka Leo hakuna kitu CCM ni jambo gani mnaeeza?
 
Habari Wana JF, naomba kuleta malalamiko yangu hapa maana najua kuna Viongozi pia wanapita kusoma taarifa zetu hapa.

Ni muda mrefu sana Barabara ya kutoka Mbezi Luis kwenda Mpiji Magohe ni mbovu sana na wenye Mamlaka wako kimya wananchi tunateseka mno.

Tumejaribu kufikisha kero Ofisi za Serikali ya Mtaa lakini hakuna msaada wowote tunaopata.



=============

Barua ya Wazi kwa Waziri Mkuu kuhusu changamoto Mbezi Luis kwenda Mpigi Magoe

Shikamoo Baba yetu na Waziri Mkuu wetu kipenzi unayesikia na kujali.

Mimi ni Mwananchi wako kutoka Mbezi Mpigi Magoe, naomba tuonee huruma, huku Watoto wa Shule na Wananchi wako tunateseka sana na Barabara.

Kuna wakati Watoto wanafika Shule Saa 3 hadi saa 4 asubuhi kwa sababu ya changamoto ya barabara.

Hii barabara ni muhimu sana na ina wakazi wengi na viongozi, pia inatoka Mbezi Stand Kuu ya Magufuli inaenda hadi Bunju.

Ni barabara mbaya sana imeharibika, gari ikikwama mnaweza kaa hata saa kadhaa za kutosha hampiti. Ndio njia ambayo kama ikitengenezwa kwa lami Mabasi ya mikoa ya Kilimanjaro na Tanga yanapaswa kupita.

Tunaomba sema neno moja kwa ajili ya hii barabara hii maana tumedanganywa na kuahidiwa uongo vya kutosha.

Tumechoka Baba. Tusikie. Ahsante. Nikutakie majukumu mema Baba.

Soma RC wa Dar, Albert Chalamila atoa maelekezo barabara zijengwe usiku na mchana
Sambamba na hiyo ni
1. barabara ya Mbezi Mwisho kwenda makabe, msakuzi, alubaba, dolphin mpk mpigi mahohe
2. Barabara ya mbezi mpaka Msumi
3. Barabara ya kwa msuguri Msingwa mpaka kifuru
 
mkuu mkoa bado sana miundombinu
 
Sambamba na hiyo ni
1. barabara ya Mbezi Mwisho kwenda makabe, msakuzi, alubaba, dolphin mpk mpigi mahohe
2. Barabara ya mbezi mpaka Msumi
3. Barabara ya kwa msuguri Msingwa mpaka kifuru
Hiyo barabara ndiyo ovyo
Wameweka lami kipande nusu mpaka kanisani hapo aise huyo mkandarasi mhuni tu
Kwengine kote ovyo tu mashimo tu

Ova
 
Hiyo barabara ilikuwa ijengwe kwa lami kuendeleza ile barabara ya Mbezi Kinyerezi. Kilichotokea sasa..... lami imepelekwa Kibamba Chama kwenda Kibwegere.
Hata hiyo barabara ya kwenda kibamba ni ya kiwango cha chini sana
 
Tatizo la Dar es Salaam nia Tanzania nzima ni sisi wananchi, serikali za mitaa na pamoja na wizara ya ardhi kutokufuata masterplan....

Kawaida maeneo yote yaliyopimwa miundombinu ya barabara, maji na umeme hupaswa kuanza kabla ya ujenzi wa nyumba yeyeto...

Lakini Bongo iko tofauti, nyumba hutangulia kwanza tena kwa ujenzi holela halafu huja umeme, maji na mwishoniiii baada ya miaka kadhaa ya uchaguzi ndio barabara hujengwa...
 
Siisiiiemuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee mitano tena kwao
 
Back
Top Bottom