Barabara ya Mbweni kwenda Boko Magengeni imefungwa!

Barabara ya Mbweni kwenda Boko Magengeni imefungwa!

Benderea

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2021
Posts
686
Reaction score
1,303
Ndugu wadau,

Ningependa wananchi wafahamu kuwa barabara muhimu inayotoka Mbweni Kijijini kupitia Malindi , masaiti hadi Boko Magengeni imefungwa !

Hii ni barabara muhimu sana hasa kwa wakazi wa Mbweni kijijini na wengineo wa njiani. Cha ajabu haieleweki kwa nini imefungwa !

Ikumbukwe kuwa hizi barabara zinatengenezwa kwa kutumia kodi za wananchi sasa inapotokea barabara inafungwa ghafla bila sababu yoyote ya msingi hili ni tatizo kubwa !

Kuna wananchi wanahitaji kusafiri , kuna wagonjwa wanahitaji kupelekwa hospitali , pia kuna bandari ndogo ya Mbweni , sasa unapofunga barabara manaake nini ??

Hivi Mbunge wetu Gwajima uko wapi ??? Diwani uko wapi ??? Ingilieni kati jamani hili suala tunataka barabara ifunguliwe na tuitumie tafadhali
 
Mkuu, barabara iliyofungwa ni ile inayopita karibu na Geti la usalama. Kama safari yako ni kuelekea mbweni kijijini, ipo barabara inayotokea pale mbweni ubungo, ni nzuri tu unaweza kutumia ile.
 
Je umejaribu kufuatilia sababu za barabara kufungwa? Au umepita imefungwa tu haraka ukaleta uzi humu? Katika hali ya kawaida haiwezekani barabara ifungwe tu bila sababu. Ambacho ungelalamikia ni kwamba barabara imefungwa na hakujawekwa barabara mbadala ya kusaidia wananch kupita lakini sio kusema imefungwa bila sababu. Yaani tu wameamua kufunga barabara ili msipite?
 
Back
Top Bottom