Barabara ya Mianzini - Ngaramtoni KM 18 Kukamilika Septemba 2025

Barabara ya Mianzini - Ngaramtoni KM 18 Kukamilika Septemba 2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

BARABARA YA MIANZINI-NGARAMTONI KM 18 KUKAMILIKA SEPTEMBA

Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Arusha Eng. Reginald Massawe kumsimamia kikamilifu mkandarasi Stecol Corporation anaejenga barabara ya Mianzini - Ngaramtoni Km 18 kuhakikisha inakamilika ifikapo Septemba mwaka huu.

Akizungumza wakati akikagua maendeleo ya ujenzi huo amesisitiza kufanyakazi usiku na mchana ili mradi huo ukamilike kwa wakati ili kurahisisha usafiri na usafirishaji jijini Arusha.

Amesisitiza ujenzi wa Barabara katika miji na majiji uendane na uwekaji taa za barabarani zinazotumia jua (solar power), ili kupendezesha mitaa na kuiwezesha kupitika wakati wote.

"Mh.Rais Samia ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya barabara jijini Arusha hivyo hakikisheni kazi inafanywa kwa ubora, hatutakubali barabara iharibike baada ya muda mfupi" amesisitiza Ulega.

Aidha, Waziri huyo amemhakikishia mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda kuwa Serikali itazijenga barabara zote unganishi na wezeshi jijini Arusha ili kupunguza msongamano wa magari na kuendana na maandalizi ya mashindano ya kombe la mataifa ya Africa AFCON 2027.

"Tutahakikisha tunaondoa msongamano kwa kuzijenga barabara zote zenye msongamano na zinazounganisha na kiwanja cha mpira" Ulega.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara jijini Arusha nakusisitiza itachochea ukuaji wa sekta ya utalii na kukuza uchumi wa watu jijini humo.

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Mohamed Besta amesema tayari Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 23 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo na wamejipanga kuhakikisha miradi ya barabara na madaraja inayoendelea mkoani Arusha itasimamiwa na inakamilika kwa wakati.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.00.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.00.jpeg
    837.2 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.10.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.10.jpeg
    812.5 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.13.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.13.jpeg
    473.4 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.17.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.17.jpeg
    438.5 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.42.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.42.jpeg
    802.9 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.51.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.51.jpeg
    610.7 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.56.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-07 at 11.06.56.jpeg
    565.3 KB · Views: 7
Back
Top Bottom