Katika miaka ya hivi karibuni, eneo la Yiling huko Yichang mkoani Hubei limeendelea kuhimiza ujenzi wa miundombinu, kwa kujenga barabara zinazounganisha vijiji vya milimani, na kuunda mtandao wa usafiri kati ya miji na vijiji, na kuwasaidia wakulima wa milimani kusafiri na kuuza bidhaa za kilimo, kuhimiza maendeleo ya kiuchumi ya maeneo ya milimani, na kusaidia uendelezaji wa maeneo ya vijijini.