KERO Barabara ya Mjimwema (Kigamboni) kwenda Dege ina makorongo sana

KERO Barabara ya Mjimwema (Kigamboni) kwenda Dege ina makorongo sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Kigamboni, na tunakabiliwa na changamoto ya barabara ya kutoka Mjimwema hadi Dege.

Barabara hii ipo karibu na makazi ya watu, na katika ukarabati wa sehemu zilizoharibika, lami huchimbwa na kuacha barabara ya vumbi kwa zaidi ya miezi sita kabla ya kurekebishwa. Hali hii imekuwa kero kwa wakazi wa maeneo hayo kutokana na vumbi linalosababishwa.

Aidha, wakati ukarabati ukikamilika, mara nyingi sehemu nyingine tayari zimeharibika, jambo ambalo linakwamisha juhudi za kuboresha barabara hiyo kwa ufanisi.

Tunaomba mamlaka husika zizingatie muda wa ukarabati ili mashimo yanapochimbwa, marekebisho yafanyike kwa haraka, na kero hii iishe.

IMG_2687.jpeg
IMG_2688.jpeg
IMG_2691.jpeg
IMG_2692.jpeg
IMG_2693.jpeg
IMG_2694.jpeg
IMG_2695.jpeg
IMG_2698.jpeg
IMG_2696.jpeg
IMG_2697.jpeg
IMG_2700.jpeg
IMG_2699.jpeg
IMG_2701.jpeg
IMG_2703.jpeg
IMG_2704.jpeg
IMG_2702.jpeg
 
Back
Top Bottom