Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
JIMBO LA MOMBA KUNUFAIKA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024
Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe amesema Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imepanga kujenga miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami katika Jimbo la Momba katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024
Barabara ya Mlowo - Kamsamba iliyopo kwenye Ilani ya CCM 2020-2025 ukurasa wa 75 ina urefu wa kilomita 145 inayounganisha Wilaya ya Mbozi, Momba na Sumbawanga Vijijini, pia inaunganisha Mkoa wa Mbeya, Songwe na Rukwa sasa imeingia kwenye bajeti na sasa itaanza kutangazwa ili iweze kutengewa fedha ambapo bajeti iliyopangwa itaanza na ujenzi wa kilomita 50 kwa kiwango cha lami
Aidha, Barabara ya Kakozi - Ilonga yenye urefu wa kilomita 51.145 kwa zaidi ya Miaka 20 iliombewa kwenda TANROAD bila mafanikio. Katika bajeti ya 2023-2024 imeweza kufanikiwa kuhama kutoka TARURA kwenda TANROAD