Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Barabara Kuu ya Morogoro-Dodoma ambayo mapema leo Septemba 5, 2024 ilifungwa na wananchi wa Mtaa wa Mkundi Sheli, Kata ya Mkundi, Manispaa ya Morogoro, kwa takriban saa mbili wakipinga ajali za mara kwa mara zinazotokea katika eneo hilo imefunguliwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Yohana Mjengi amewataka wananchi hao kuwa wavumilivu na kuepuka kuchukua sheria mkononi pia kuacha kufunga barabara na kueleza kuwa Jeshi la Polisi linafuata taratibu na sheria katika kushughulikia matatizo ya usalama barabarani.
Wananchi hao walifunga barabara hiyo baada ya malalamiko ya muda mrefu ya ajali zinazodaiwa kusababishwa na madereva wa mabasi na magari makubwa hususani ya mizigo yanayopita katika barabara hiyo.