Barabara ya Mwenge-Tegeta itaisha lini?

Barabara ya Mwenge-Tegeta itaisha lini?

Status
Not open for further replies.

Maundumula

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
7,553
Reaction score
3,081
Habari wandugu,

Hii barabara yetu ya Mwenge-Tegeta mbona muda unakwenda bado hatuoni matumaini. Jamaa wapo Tegeta wanajenga daraja at snails pace imeshachukua mwaka mzima. Hapo mwenge napo hata dalili ya kumalizia kile ki daraja hamna.

Pale Golden Bridge njia panda ya kawe wamejenga upande mmoja bado hawajafungua na hawana mpango wa kufungua.

Kwa anayefahamu muda wa kukamilika huu mradi naomba atufahamishe tujue. Kila siku foleni btn Africana na Kunduchi njia panda. Tumechoka kufika majumbani saa sita za usiku na kuamka saa kumi!
 
bandugu,haya mambo inabidi uwe na imani ya kipofu kuona..ukitaka soma bango la mradi liko mwenge hapo
au utafute info TANROADS....
 
bandugu,haya mambo inabidi uwe na imani ya kipofu kuona..ukitaka soma bango la mradi liko mwenge hapo
au utafute info TANROADS....
Bango linaonesha walitakiwa kukamilisha kazi mwezi huu (May 2013). wamefungua njia moja nyingine wamefunga wakati hafanyi kazi yeyote.. wameshatuchosha sana hawa jamaa.
 
Kama mradi ulitakiwa uishe May 2013 inakuaje Magufuli wakati anajibu swali la mbunge wetu amesema kuwa mradi unaenda vizuri hauendi kwa kusuasua?
 
Bango linaonesha walitakiwa kukamilisha kazi mwezi huu (May 2013). wamefungua njia moja nyingine wamefunga wakati hafanyi kazi yeyote.. wameshatuchosha sana hawa jamaa.
Mkuu kalisome upya bango. Tarehe imebadilika. Ni August 31st.
 
Naona sasa wamefungua kidogo pale njia panda ya kawe sema ndio imekuwa balaa maana hapaeleweki njia 3 au 2.
 
Habari wandugu, Hii barabara yetu ya Mwenge-Tegeta mbona muda unakwenda bado hatuoni matumaini. Jamaa wapo Tegeta wanajenga daraja at snails pace imeshachukua mwaka mzima. Hapo mwenge napo hata dalili ya kumalizia kile ki daraja hamna. pale Golden Bridge njia panda ya kawe wamejenga upande mmoja bado hawajafungua na hawana mpango wa kufungua. Kwa anayefahamu muda wa kukamilika huu mradi naomba atufahamishe tujue. Kila siku foleni btn Africana na Kunduchi njia panda.Tumechoka kufika majumbani saa sita za usiku na kuamka saa kumi!!!

Sababu ya kukufanya ufike nyumbani saa Sita usiku unaijua mwenyewe ila umeamua kutumia ma------ kutudanganya eti ni Ujenzi wa barabara unaoendelea!
 
Je bado kuna dalili za project kukamilika hiyo August 31?
 
Habari wandugu,

Hii barabara yetu ya Mwenge-Tegeta mbona muda unakwenda bado hatuoni matumaini. Jamaa wapo Tegeta wanajenga daraja at snails pace imeshachukua mwaka mzima. Hapo mwenge napo hata dalili ya kumalizia kile ki daraja hamna. pale Golden Bridge njia panda ya kawe wamejenga upande mmoja bado hawajafungua na hawana mpango wa kufungua. Kwa anayefahamu muda wa kukamilika huu mradi naomba atufahamishe tujue. Kila siku foleni btn Africana na Kunduchi njia panda.Tumechoka kufika majumbani saa sita za usiku na kuamka saa kumi!!!

Vuta subira mkuu
 
August si ndo hii, kuna matumaini ya kuisha hiyo 31st?
Nimetonywa kuna mvutano kati ya mkandarasi, wacoraji na wasimamizi wa mradi, na TANROADS kwa pande tatu.
Kazi iko chini ya kiwango cha uchoraji na hata usimamizi.
kuna sehemu zitarudiwa kwa gharama za mkandarasi.

Kiujumla usanifu wa kazi yenyewe ni mbaya na sijui TANROADS walikuwa wapi, kuuziwa mbuzi kwenye kiroba!
 
Mimi sio mhandisi ila kwa kungalia jinsi ile mitaro ilivyojengwa ukilinganisha na barabara hata ahaviendeani. Kawaida mtaro huanzia lami inapoishia.
 
Kwa kweli kama kuna barabara ambayo tunaibiwa tunaona na ambayo inaleta mateso kwa watanzania ukiacha hiyo ya Morogoro ni hii. Sielewi hata aliyebuni hivyo vituo vya daladala alifikiri nini! Kwa kweli "Za wajinga huliwa mwerevu" Wabongo hatujitambui!!!
 
Vile vituo ni vyembamba sana, kwa hawa vichwa maji wanaoendesha madaladala, foleni na ajali havitakwepeka.

Afu sioni service road kwenye baadhi ya maeneo.
 
Vile vituo ni vyembamba sana, kwa hawa vichwa maji wanaoendesha madaladala, foleni na ajali havitakwepeka.

Afu sioni service road kwenye baadhi ya maeneo.

Hii barabara ni mateso.
Hata haieleweki kazi ipi bado na ipi imekwisha. Leo mnaweza kuruhusiwa kupita lane ya kushoto kwamba ujenzi umekwisha, kesho tena mnazuiwa.

Hayo madaraja ndiyo kichekesho, kama lile la Mwenge kila siku wanajenga. Nchi hii kama ina laana, kama hayo yanafanyika kwenye mji wenye Viongozi wote wakuu, sijui huko mikoani hali ikoje!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom