Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
BARABARA YA NANENANE - TUNGI MOROGORO KUFANYIWA UKARABATI MWAKA MPYA WA FEDHA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Waziri Mzeru katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni ameuliza swali Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi juu ya mpango wa Serikali kukarabati barabara mkoani Morogoro
"Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati barabara kutoka Nanenane - Tungi kupitia VETA kwa kiwango cha lami Mkoa wa Morogoro"? - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro
"Tumekuwa na utaratibu wa kufanya matengenezo ya Barabara zote kwa kiwango cha lami. Mwaka unaokuja wa fedha tumetenga fedha kwa ajili ya kukarabati maeneo yote yaliyoharibika ili barabara irudi kwenye ubora wake" - Mhe. Geoffrey Kasekenya, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
Awali, wananchi wa Mkoa wa Morogoro waliwasilisha ombi lao kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Mhe. Norah Waziri Mzeru juu ya ahadi ya muda mrefu waliyopewa juu ya ujenzi wa Barabara ya Nanenane - Tungi kupitia VETA
"Mheshimiwa Mbunge, pole na majukumu Mheshimiwa wakazi wa Kata ya Tungi kero yetu kubwa ni barabara ya kutoka Nanenane, Tubuyu, Tungi mpaka VETA tumeaidiwa muda mrefu kujenga kwa kiwango cha lami tunapata tabu kubwa ya usafiri Tunaomba utusaidie kufuatilia na sisi tufuraie kuwa na barabara ya lami ni aibu barabara hii ndani ya manispaa laki utafikiri ni kijijini" - Mwananchi