carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Tanga umetangaza Barabara Kuu ya Tanga – Segera itafungwa leo kwa saa nne.
Meneja wa Tanroads wa Mkoa, Msama Kosani amesema barabara hiyo itafungwa kuanzia asubuhi hadi saa sita mchana ili kuruhusu ukarabati wa madaraja ya Hale na Maguzoni.
Kosani alisema juzi wataalamu wa Tanroads walikagua barabara na madaraja mkoani humo na kubaini changamoto zinazohitaji kushughulikiwa haraka kufuatia taarifa za uwezekano wa kunyesha mvua nyingi za vuli zinazotarajiwa kuambatana na El Nino.
Alisema ukarabati huo utahusisha maeneo ya chini ya madaraja yanayopitisha maji pamoja na vyuma vya juu vilivyoanza kupata kutu kutokana na maji ya mvua, hatua inayolenga kuimarisha uimara wa madaraja hayo na kulinda usalama wa watumiaji wa barabara.
Kosani alisema Tanroads imejipanga kuhakikisha vifaa na mitambo vinafika eneo la kazi na ukarabati unakamilika kwa wakati.
Alisema Barabara ya Tanga-Segera ni kiunganishi muhimu kwa magari kutoka Dar es Salaam kupitia Chalinze kwenda Tanga na Segerea pamoja na magari kutoka mikoa ya Singida, Arusha na Kilimanjaro.
Chanzo: Habari leo