KERO Barabara ya Ubungo makoka kutokea Riverside kupitia kwa Mzee wa Upako inaenda miezi minne mpaka sasa hakijamalizika

KERO Barabara ya Ubungo makoka kutokea Riverside kupitia kwa Mzee wa Upako inaenda miezi minne mpaka sasa hakijamalizika

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Tile

New Member
Joined
Mar 9, 2024
Posts
3
Reaction score
5
Wakuu kwenye hii barabara ya kwenda Ubungo Makoka kupitia kwa Mzee wa Upako, kuna kipande kama mita 300 kinaongezwa kwa kiwango cha lami inaenda miezi minne mpaka sasa hakijamalizika.

Jamaa wakijisikia wanafunga barabara hamna gari kupita, njia mbadala ni milimani na ndogo magari hayapishani.

Kama saivi imefungwa siku ya tatu na hamna kazi inaendelea, wahusika tafadhali walitazame hili wananchi wanateseka.

Asante
 
Kwanza sijui wanashindwaga nini kuimalizia tu iyo barabara. Walianza mita 400 kutoka pale kilimani. Sahivi sijui mita 100 hapo Unyamwezini. Watakuja mita 200 hadi shule ya msingi pale hivo hivo hadi 2030 ndio inakutana na ile ya Maji Chumvi.
 
Ukute hela za ujenzi zimeshaingia mifukoni mwa wajanja. Sasa mkandarasi anashindwa kuendelea na ujenzi bila kulipwa.
Hizi hukuIlisikika sauti "Shikilieni picha ili mpigwe picha,hakikisheni sura zenu hazionekani" wakasahau kuficha miguu😀😀
 
Attachments

  • IMG-20241012-WA0105.jpg
    IMG-20241012-WA0105.jpg
    67.6 KB · Views: 5
Wakuu kwenye hii barabara ya kwenda Ubungo Makoka kupitia kwa Mzee wa Upako, kuna kipande kama mita 300 kinaongezwa kwa kiwango cha lami inaenda miezi minne mpaka sasa hakijamalizika.

Jamaa wakijisikia wanafunga barabara hamna gari kupita, njia mbadala ni milimani na ndogo magari hayapishani.

Kama saivi imefungwa siku ya tatu na hamna kazi inaendelea, wahusika tafadhali walitazame hili wananchi wanateseka.

Asante
Weka evidence tuona mtu wa maana kabisa😃
 
Washenzi hela washachukua wanakula bata kwanza sasa hivi wanajua hakuna mtu wa kuwauliza kitu chochote hata wasipojenga mpaka Yesu arudi

Kuna sehemu nipo jamaa wanajituma sana kujenga barabara ingawa hivyo hivyo kwa vifaa vya kuungaunga ila wanajenga na barabara inajengwa, nilimkuta jamaa usiku analilia hela ya mafuta ya shindilia ili mapema ashindilie barabara jamaa anaemwambia aingize hela muda huo yeye yupo club wakati yeye yupo kwenye shindilia analala nalo mpaka kunakucha, kesho yake jioni napita nakuta jamaa kashamaliza kazi tayari

Kwa hio hao wakuda hela wamepewa na muda huu wapo club wanabambia warembo kwanza
 
Nchi ina wajinga sana hii mkuu.
Wajinga hawawezi kuisha ila wajinga namba 2 ni hao wanaofunga barabara halafu hawaitengenezi wanakula bata kwanza mpaka hela iishe yote ndio waje kuweka magepu magepu baadae muwaite waje kufukia viraka kwenye mashimo barabara ishakua mbovu haifahi mnakumbuka miaka 2/3 nyuma kuna wapuuzi walifanya ujinga wao hapo
 
Ndio, na haya yanafanyika kwa vile hakuna wafuatiliaji. Ingekuwa Rwanda huu ujinga usingetokea.
 
Ndio, na haya yanafanyika kwa vile hakuna wafuatiliaji. Ingekuwa Rwanda huu ujinga usingetokea.
Hakuna mtu anasema kabisa ataniuliza nani sawa hata akiniuliza atanifanya nini? Hana cha kunifanya anakwangua mpunga huyooo club akale bata kwanza
 
Updates…
Mpaka leo siku ya saba ,barabara bado imefungwa na hakuna kazi inaendelea
 
Back
Top Bottom