Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
JIMBO LA KITETO - EDWARD OLE LEKAITA
TAARIFA MAALUM KUHUSU UJENZI BARABARA ZA LAMI
BARABARA KONGWA - KITETO- SIMANJIRO- ARUSHA KM 453
BARABARA HANDENI - KITETO- NCHEMBA - SINGIDA KM 460
Ndugu wananchi wenzangu wa Jimbo la Kiteto najua wengi wenu mmekuwa mnanipigia simu kuhusu Ujenzi wa Barabara yetu ya Kongwa - Kiteto - Simanjiro- Arusha KM 453 na Barabara ya Tanga- Kibirashi - Kijungu - Kibaya- Chemba - Singida ( KM 460) kuwa ni lini haswa Barabara hizi zitajengwa kwa kiwango cha Lami. Napenda kuwafahamisha kuwa kutoka na Kilio chetu kuhusu Barabara hizi mbili kuu kupitia kwa sauti yenu Bungeni Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwamba Barabara zetu hizi mbili zitajengwa kwa kiwango cha LAMI.
Ndugu wananchi wenzangu Leo asubuhi tarehe 18.5.2023 nimeuliza swali kwa Mhe. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi nikitaka kujua ni lini hasa Mikataba ya Ujenzi wa Barabara hizi utafanyika na kama wanaweza kuja Kiteto kwaajili ya Kusaini Mkataba huu.
Leo pia baada ya Swali langu kujibiwa vizuri nimepata nafasi ya kuzungumza na Mhe. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa na amenifahamisha kuwa kwa kuwa Barabara ya Tanga - Kibirashi - Kiteto - Chemba - Singida ni KM 460 na kwa kuwa Barabara ya Kongwa - Kiteto- Simanjiro- Arusha KM 453 yaani Jumla ya KM 913 na barabara zingine jumla yote KM Kilometa zaidi ya 2000 kwa kuwa ni miradi mikubwa mno Wizara imeona ni vyema Mikataba hii ikasainiwa mbele ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan halfa ambayo inatarajiwa kufanyika Mwezi wa 6 2023 kwa tarehe tutakayopangiwa kutokana na ratiba za Mhe. Rais.
Ndugu wananchi wenzangu ni dhahiri kuwa Barabara hizi mbili kubwa za LAMI zitafungua wilaya yetu kiuchumi. Nawaomba tujiandae vyema ili fursa zitakazoletwa na Barabara hizi mbili zilete faida kubwa chanya kwetu.
Nawaomba tuendelea kumwombea Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini kwa moyo wa kuendelea kutufuta pesa kwaajili ya miradi ya kuboresha Miundombinu ya Barabara za Lami kwaajili ya kushughulia changamoto.