Barabara za zege zinadumu na gharama nafuu kuliko za lami kwanini nchi nyingi za Africa wanapendelea lami?

Barabara za zege zinadumu na gharama nafuu kuliko za lami kwanini nchi nyingi za Africa wanapendelea lami?

Gharama ni kubwa sana kwenye zege lakini pia zege kufanya maintenance ni gharama kubwa,
Asphalt ni rahisi kwa bei, ni rahisi kwenye matengenezo
 
Barabara za zege zinadumu na ghalama nafuu kuliko za lami kwanini nchi nyingi za Africa wanapendelea lami?
Sio ghalama ni gharama.

Zege ni more expensive kuliko lami...

Nimekuwekea ufafanuzi hapa chini kwa km 1 ya ujenzi.

1. Gharama ya awali/km
TZS 1.5B – 2.5B - Lami
TZS 2.5B – 4.0B -zege
2. Maisha ya barabara
Miaka 15-20 lami
Miaka 30-40 zege
3. Matengenezo/mwaka
Ghali — TZS 50-100M - lami
Nafuu — TZS 20-40M - zege
4. Gharama ya maisha yote
Ghali zaidi mwishowe - lami
Nafuu zaidi mwishowe - zege
5. Wakati wa kujenga
Haraka - Lami
Polepole zaidi - zege
 
Initial cost ya barabara ya zege usipime. Zege inaenda pamoja na nondo na ndicho kinachopandisha gharama.
 
Lami huaribika haraka kuliko za zege, kwa standard ya barabara inayofanana, za zege ni ghali kuliko za lami.

Lakini pia lami inatoa smooth drive kuliko zege😀😀
Asante sana Mhandisi
 
Back
Top Bottom