Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. ORAN NJEZA - BARABARA ZILIZOPANDISHWA HADHI ZIWEKEWE LAMI MBEYA VIJIJINI
"Je, lini barabara ya Ilambo - Nsonyanga inayounganisha Barabara ya Isonje - Makete - Njombe - Tanzaki itapandishwa hadhi"? - Mhe. Oran Manase Njeza, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini
"Tarehe 09 Januari 2023 kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Mbeya kilifanyika ambapo moja ya Barabara zilizopendekezwa kupandishwa hadhi ni Barabara ya Ilambo - Nsonyanga yenye urefu wa kilomita 22. Kamati ya Kitaifa ya kupanga Barabara katika hadhi stahiki NRCC ilifanyika Mkoa wa Mbeya tarehe 24 Februari 2023 na kutembelea Barabara zilizoombwa kupandishwa hadhi ikiwemo Barabara ya Ilambo - Nsonyanga.
Mapendekezo ya Kamati yaliwasilishwa kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na yanachambuliwa, uchambuzi ukikamilika taarifa itatolewa" - Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI
"Kwa vile Barabara ipo kwenye hali mbaya sana, Ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ili ianze kupitika"? - Mhe. Oran Manase Njeza, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini.
"Kuna Barabara ya Ilembo - Isonzo ambayo inaunganisha Mkoa wa Mbeya na Mkoa wa Songwe. Je, ni lini Barabara hii itapandishwa hadhi kuwa ya Mkoa?" - Mhe. Oran Manase Njeza, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini
"Barabara ikishakuwa imekidhi vigezo vya kupandishwa hadhi na kuwa inahudumiwa na TANROAD basi ni wajibu wa TANROAD kutenga bajeti hiyo kuweza kutengeneza Barabara. Tutakaa na wenzetu wa Ujenzi kuona wamejipanga vipi kwa ajili ya kutengeneza Barabara" - Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI.
"Barabara ya Ilembo - Isonzo itapandishwa hadhi baada ya kutimiza vigezo vya kisheria kama ambavyo Barabara zingine wanafanya. Waanze vikao vyao katika DCC, RPC, Bodi ya Barabara ya Mkoa na kisha kumuandikia Waziri wa Ujenzi mwenye dhamana na Barabara za Mkoa" - Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI.