Che Kalizozele
JF-Expert Member
- Jul 20, 2008
- 777
- 50
Barafu/ice ni maji (peke yake) yameganda wakati ice cream ni maji yamechanganywa na maziwa (au kitu kingine)
Kimatumizi; barafu/ice unapoozea maji wakati ice cream wailamba yakhe ndio maana ice cream huku kwetu inaitwa lamba lamba.
Lakini kule kwenu kwa kuwa mnalamba hata ice/barafu- basi zote (ice na ice cream) mwaziita lamba lamba.
Maoni yangu.
Kuna barafu ambayo inatoka na uchanganyaji wa maziwa na maji na radha kidogo ya kahawa ama iriki ama maji na ukwaju, na inaweza kuongezwa rangi ili kuvutia inaitwa Malai.
Mara nyingi husikia watoto wakisema ashikrimu wakitaka hizo lambalamba (wengine husema rambaramba hichi si kiswahili sahihi neno kuu ni Lamba na sio ramba)
Lamba inamaana ya kula kutumia ulimi kwa mtindo wa kutembeza ulimi ama kinacholiwa kwa kupakaza ulimi.
Baba Wa3 kuna maneno umeyatumia huwa yananichefua kidogo nikikutana na mtanzania mtumiaji wa kiswahili akiyatamka mfano
unitatiza badala ya Hunitatiza (ukiacha ile herufi H basi maana inabadilika na kumtatiza msomaji/msikilizaji)
vilevile kwa maneno "umaanisha" usahihi wake ni humaanisha.
Mkuu kibunango hebu tizama/tazama maneno niliyoyatilia rangi uniambie yakoje masikioni mwa msikilizaji
'Kuna barafu ambayo inatokana na uchanganyaji wa maziwa na maji na radha kidogo ya kahawa ama iriki ama maji na ukwaju, na inaweza kuongezwa rangi ili kuvutia inaitwa Malai.'
lengo langu sio linginelo zaidi ya kutaka tujitahidi kutumia kiswahili vizuri zaidi kwa kadri tuwezavyo ili tuweze kuwafunza na wengine kiswahili kizuri.
Sawa sawa tupo pamoja katika hilo.lengo langu sio linginelo zaidi ya kutaka tujitahidi kutumia kiswahili vizuri zaidi kwa kadri tuwezavyo ili tuweze kuwafunza na wengine kiswahili kizuri.
Mara nyingi husikia watoto wakisema ashikrimu wakitaka ..............QUOTE]
Nakubaliana na wewe mkuu: 'Aiskrimu' au 'Ashikirimu' yote yamepata mashiko baina ya wazungumzaji wa kiswahili (wa bara). Kwa Unguja, neno 'malai' linatumika zaidi.
Mara nyingi husikia watoto wakisema ashikrimu wakitaka hizo lambalamba (wengine husema rambaramba hichi si kiswahili sahihi neno kuu ni Lamba na sio ramba)
Lamba inamaana ya kula kutumia ulimi kwa mtindo wa kutembeza ulimi ama kinacholiwa kwa kupakaza ulimi.
Baba Wa3 kuna maneno umeyatumia huwa yananichefua kidogo nikikutana na mtanzania mtumiaji wa kiswahili akiyatamka mfano
unitatiza badala ya Hunitatiza (ukiacha ile herufi H basi maana inabadilika na kumtatiza msomaji/msikilizaji)
vilevile kwa maneno "umaanisha" usahihi wake ni humaanisha.
Mkuu kibunango hebu tizama/tazama maneno niliyoyatilia rangi uniambie yakoje masikioni mwa msikilizaji
'Kuna barafu ambayo inatokana na uchanganyaji wa maziwa na maji na radha kidogo ya kahawa ama iriki ama maji na ukwaju, na inaweza kuongezwa rangi ili kuvutia inaitwa Malai.' lengo langu sio linginelo zaidi ya kutaka tujitahidi kutumia kiswahili vizuri zaidi kwa kadri tuwezavyo ili tuweze kuwafunza na wengine kiswahili kizuri.
Nilipokuwa shule ya msingi, dio nilianza kulisikia neno Malai (ice cream), toka kwa watoto wa kipemba.