Ugonjwa wa Corona Virus au Covid-19 inazidi kuleta madhara na kusababisha vifo mbali mbali duniani na hapa nchini.
Bila shaka nchi yetu ndo miongoni mwao nchi chache barani Afrika ambazo zimechukua tahadhari kadhaa bila kufungia wananchi wake ndani (Lockdown) na kuacha wananchi waendelee kufanya shughuli za uzalishaji huku wakihadhari.
Kutokana na hali kuonekana kuanza kuwa mbaya kutokana na idadi kubwa ya watu wanaotangazwa kwa sasa, Hospitali na vituo vya afya zimeanza kutoruhusu wagonjwa kuingia Getini la Hospitali bila kuwa wamevaa Barakoa. Hili ni jambo la kupongezwa na la maana sana kujilinda na maabukizi.
Hata hivyo, hali ya barakoa moja kuuzwa Tshs 2000 imekuwa kidogo changamoto kwa wagonjwa hasa walala hoi. Je hakuna uwezekano bei ikapungua angalau ikauzwa kwa rejareja tshs 500? Kwa kweli hili nalo ni janga.
Hakuna mtu anayependa kuugua huu ugonjwa au kuambukiza wengine huu ugonjwa. Sasa kama vifaa vya kujikinga vitakuwa bei ghali je wananchi wa hali ya chini watamudu?
Tunakoelekea, itakuwa kwamba huwezi ingia sokoni bila kuvaa barakoa[emoji40] nalo ni jambo jema sana na kama watendaji wanaliona mapema na kianze maana masikini nako japokuwa tunanawa mikono basi watu tuvae na barakoa kujilinda kikamilifu. Iwe lazima kwa muuzaji na mteja kuvaa barakoa.
Barakoa inashauliwa kuvalia kwa masaa 4 mfululizo na baada ya hapo itolewe na mtu avae nyingine. Je kama zitakuwa zinauzwa Aghali je wananchi watamudu?
Leo hii pale St. Joseph Hospital Mjini moshi, kuna watu walikuwa wamekwama kuingia mlangoni mwa geti la hospitali kwa kukosa 2000 ya barakoa.
Si kila aende hospitali anaumwa, wengine huwapelekea chakula ndugu zao wagonjwa waliolazwa. Sasa kama mtu alikuwa amejiandaa na nauli halafu anakuta stop getini ya kotoingia bila kuvaa barakoa hapo huwa mtihani.
Kama mama amempeleka mtoto kwenye matibabu, hapa inamlazimu kununua barakoa Mbili : ya kwake (mama) na mtoto pia.Kwa hali hiyo mama atagharamia sh 4000. Hii gharama hakuitegemea kabisa!
My takes.
Barakoa zigawe bure au zipungue bei na zivaliwe na kila mtu sehemu ya mkusanyiko.
Kwa sasa si muda wa Hospitali na maeneo ya public ya mkusanyiko kufanya biashara za hizi Barakoa kama ilivyo kwenye Hospitali ya St. Joseph Mjini Moshi. Wazitoe kama huduma na kama inagalimu basi zitolewe kwa bei nafuu sana.