Barakoa 😷 Kujilinda na COVID-19 zauzwa Tshs. 2000 na Bila kuivaa huingii lango la Hospitali kwenda kupata matibabu

.... hongera ndg umetoa elimu njema Sana nazani wahusika wakilifanyia kazi inaweza saidia sana....lengo kuu ni kuondoa maambukizi mapya na kuendana na hali ya vipato vya wananchi.....
 
Balakoa zinatengenezeka, kama kweli unahitaji kuvaa na kujilinda, si lazima ununue.
Ukiwa na lesso ukaikunja vizuri na rubber band zako tayari balakoa.
Wale akina mama wa kiislam hawahitaji ziada tena, lile vazi tosha kabisa.
Hiyo ya massa manne ni kwa wale wanaohisi imezidiwa jasho mate nk
 
Kama inatakiwa kuvaliwa kwa masaa 8 tu,ina maana kwa siku mtu unatakiwa utumie Barakoa 2 hasa kwa sisi tunaokwenda kwenye mihangaiko ya kutafuta pesa,hiyo ina maana tayari ni 4,000.00...!!
Mkuu acha kupotosha!
 
aisee hii ni mpya ...nimepata sasa kutoka kwako
 
Pesa za kununua ndege tungepata barakoa hadi tukazikimbia
....nikweli lakini kwasasa ndege tulikwisha nunua hata tukisema tuuze ili tupate pesa ya barakoa hatuwezi kupata mteja....nazani tuanze na vilivyopo (1) wabunge wapunguze posho na mishahara yao iyo pesa isaidie kununua barakoa (2) mh: rais waziri mkuu na mawaziri wote wapunguze mishahara yao isaidie kununua barakoa (3) wakuu wote wa idara wakuu wa mikoa na wilaya makatibu na watendaji wote wapunguze mishahara na posho iyo pesa isaidie kununua barakoa (4) ruzuku ya vyama vya siasa vyote ipunguzwe nusu ikasaidie kuwalipia wananchi umeme na maji katika kipindi hiki kigumu cha mapambano ya covid-19
 
Kama inatakiwa kuvaliwa kwa masaa 8 tu,ina maana kwa siku mtu unatakiwa utumie Barakoa 2 hasa kwa sisi tunaokwenda kwenye mihangaiko ya kutafuta pesa,hiyo ina maana tayari ni 4,000.00...!!
Kuna barakoa za aina tofauti Kuna zile ambazo unavaa na kuzifua yaani kuzifanyia usafi( reusable mask) na hizo za muda mfupi ( disposable mask) na Bei hazifanani,ukiona huwezi ya 2000 unaangalia uwezo wako ili mradi kupunguza maambukizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.... hongera ndg umetoa elimu njema Sana nazani wahusika wakilifanyia kazi inaweza saidia sana....lengo kuu ni kuondoa maambukizi mapya na kuendana na hali ya vipato vya wananchi.....
Kusema kweli inasikitisha sana kuona tunaleteana usumbu kwenye jambo hatari kama hili. Ushahidi gani tunataka hili tuchukue hatua mapema?

Kuna nchi zilidharau sasa hivi wanakiona cha moto. Sisi tumshukuru Mwenyezi Mungu mpaka sasa hali ni salama kwahio ni muhimu kuanza kujikinga sasa hivi.
Juzi nilileta mada hapa kuomba rais aweke sheria ya mda watu wavae mask wakiwa kwenye miangaiko ya kila siku na kama hawataki wakae ndani. Kuna wapuuzi walinishambulia kwamba nataka niuze mask, hivi kweli kwa akili yetu ndogo kuna kitu gani kwenye mask kinamlazimisha mtu anunue kama hana uwezo kama si uvivu wa kufikiri? Mitambala yote ndani ya nyumba, kanga zote hizo na vilemba mtu anashindwa kutumia kuziba mdomo na pua anapotoka nje kuokoa maisha yake na wengine?

Tujikinge, tuoshe mikono mara kwa mara kuokoa maisha yetu ndugu zangu. Janga hili alichagui maskini wala tajiri. Tusisubiri misaada ya mask kutoka nje, wao wenyewe hawana za kutosha. Tutumie vitu tulivyokua navyo majumbani kwetu.
 
aisee hii ni mpya ...nimepata sasa kutoka kwako

kama umefanya kazi maabara ndiyo maana huwa hazitumiki kuzuia harufu wala kemikali. hutumika mara nyingi kwenye vumbi, kitaalamu vumbi lina particulates. CORONA hubebwa na particulates au droplets ambazo kwenye kitambaa hazipiti.
Hakikisha kitambaa chako hakina matundu.
 
Mungu wetu yu anatupenda sotee....wenye pesa mnunue hzo balakoa tusiokuwa na pesa tuamini tu Mungu yu pamoja nasi sote anatupenda sanaa...
 
Mkuu sema wewe. Akili zetu zimeshikwa na mchina mpaka tunashindwa kutafuta mbinu mbadala kwenye mambo madogo sana. Kila mtu analalamika bei kama wamelazimishwa kununua.
 
Hapana kwenye barakoa tusingewaza hio kitu kwanza kwenye afya msisitizo huwa dawa zaidi kisha vifaa vingine vinafatia, just imagine nchi kama marekani inafikia hatua ya kuteka barakoa za nchi nyingine. Je walizonazo hazitoshi?maskini sie tusingeweza
Hapo ndipo tungekuwa na huduma nzuri hata barakoa zingekuwa za kutosha kwa wakati fulani.
 
1.umeandika kanakwamba ni utaratibu wa hospitali zote nchini kumbe ni kwenye hiyo hospitali ya Moshi pekee (tena ya mtakatifu-siyo ya umma)

2.barakoa ni vyema zivaliwe na wagonjwa tu au kama na wengine basi kwenye maeneo hatarishi

3.usiione watu wajinga kusema msivae barakoa hovyohovyo kwani endapo mkiamua wote mvae itakuwa kama fashion na si kinga tena na ndo tutapukutika kama kuku wenye kideli maana umakini utakosekana pia itakuwa ngumu kutofautisha wagonjwa na wasio wagonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…