Barakoa 😷 Kujilinda na COVID-19 zauzwa Tshs. 2000 na Bila kuivaa huingii lango la Hospitali kwenda kupata matibabu

Nunueni barakoa za kitambaa ambazo zinafulika. Ukiwa nazo mbili au tatu zinatosha. Unafua na kubadilisha kila siku..na bei yake ndo hiyo hiyo elfu mbili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unavaa barakoa, unaenda kushika sehem yenye kirusi unajifikicha macho kidogo, tayari umekwisha!

Tuvaeni ma helmet tu yale ya pikipiki yenye kufunika kichwa kizima
 
Nimeenda hospitali leo pale Mnazi Mmoja hakuna kuchekiwa wala nini zaidi ya kupuliziwa maji yenye dawa tu .

You'd think a hospital of all places wangekua strict ila waapi . Si Madokta wala manesi waliovaa hizo mask
Wewe mbona haupo strict nyumban kwako?
 
Ila tungekuwa na huduma bora za afya ika sasa ni Mungu tu!
Hapana kwenye barakoa tusingewaza hio kitu kwanza kwenye afya msisitizo huwa dawa zaidi kisha vifaa vingine vinafatia, just imagine nchi kama marekani inafikia hatua ya kuteka barakoa za nchi nyingine. Je walizonazo hazitoshi?maskini sie tusingeweza
 
Hizo barakoa za kutoa bure kwa watu takribani millioni 40 watazipata wapi?

..siyo lazima ziwe milioni 40.

..hivi serikali haina uwezo wa kutoa barakoa kwa polisi, bodaboda, wachuuzi wa sokoni, mama ntilie, etc etc?

..kama tunaweza kutoa chanjo mbalimbali kwanini tushindwe kutoa barakoa?
 

1. Hata hospitali za umma wametoa maagizo hakuna mtu kuingia maeneo yao bila barakoa.

2. Barakoa ni nzuri na zinahitajika wakati huu. Zingekuwa hazina msaada basi madaktari na wauguzi wasingekuwa wanazitumia.

3. Katika hali iliyopo sasa hivi, ili covid19 isisambae, wenye ugonjwa, na wasio na ugonjwa, wanatakiwa wavae barakoa.

4. Barakoa zikiwa fashion au utamaduni wetu itakuwa vizuri zaidi. Hata tukiendelea na utaratibu wa sasa wa kuosha mikono itakuwa jambo jema vilevile. Tutafanikiwa kupunguza magonjwa mengi yanayosambaa kwa pumzi, au yanayosambaa kupitia mikono michafu.
 
Kuna nyumbu wa Ufipa anaweza kuonhea chochote tofauti na Mbowe na akabaki salama? Nipo mfano.

..ccm kila mtu anadukuliwa.

..bado viongozi wenu wana mawazo ya kikatili ya enzi za ukomunisti.
 
Serikali Ina viwanda 4999
Ikiwemo vya nguo kwann isitutengenezee barakoa na itupe
Bureee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…